Watu 13 wauawa Afghanistan, UN yalaani
Watu 13 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kujilipua lililofanyika leo huko Jalalabad nchini Afghanistan.
Watu 13 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kujilipua lililofanyika leo huko Jalalabad nchini Afghanistan.
Wakati wanawake barani Afgrika leo wakiadhimisha siku ya “Wanawake Afrika” iliyobeba kaulimbiu ‘’mtazamo na ubunifu” wamepongezwa kwa juhudi zao za kuchangia maendeleo barani humo.
Kila hatua inayopigwa kuelekea amani nchini Afghanistan ni muhimu sana kwa sasa kulliko wakati mwingine wowote ulee. Wito huo umetolewa leo na viongozi wa kijamii katika mdahalo unaoungwa unaofanyika mkoa wa Kusini wa Kandahar nchini humo na kuungwa mkono na Umoja wa wenye lengo la kumulika mbinu za kutanzua mgogoro na kujenga mshikamano wa jamii.
Bangladesh isitishe mara moja miradi yake ya viwanda kwenye msitu wa akiba wa Sundarbans ambao msitu mkubwa zaidi duniani wenye mikoko, amesema mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mazingira, John H. Knox.
Umoja wa Mataifa una wasiwasi kutokana na visa vinavyoendelea nchini Saudi Arabia vya kuwakamata kiholela watetezi wa haki za binadamu pamoja na wanaharakati nchini humo ikiwemo wale wanaotetea haki za wanawake.
Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la kutisha lililofanywa na magaidi wa ISIL kwenye maeneo yanayokaliwa na raia wengi huko jimbo la As-Sweida kusini-magharibi mwa Syria.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, leo limetoa wito wa mshikamano wa kimataifa na msaada kwa ajili ya Costa Rica na nchi zingine zinazo wahifadhi wakimbizi na waoomba hifadhi kutoka Nicaragua, wakati maelfu wakifungasha virago kukimbia shinikizo la kisiasa, machafuko na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa bado watoto wanakumbwa na changamoto kubwa ya kunyonya maziwa ya mama zao pale tu wanapozaliwa. Hata kwenye hospitali zenye wataalamu wabobezi bado watoto wananyimwa haki yao hiyo ambayo ni muhimu ili kuchagiza makuzi yao.
Mkaa, mkaa, mkaa tena mkaa utokanao na miti unatajwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa sababu watu wanakata miti na hivyo kuharibu misitu. Misitu ni muhimu siyo tu katika kuweka bayonuai inayohitajika na lishe kwa binadamu, Wanyama na mimea, bali pia hufyonza hewa ya ukaa ambayo inazidi kuongeza ukubwa wa tundu la ozoni kwenye anga kuu.
Nchini Mali uchaguzi wa rais umefanyika kwa amani licha ya kuripotiwa kwa visa vya hapa na pale vilivyokwamisha upigaji kura kufanyika katika baadhi ya vituo.