Mpango wa kusaidia Sahel wazinduliwa leo, utajiri wa ukanda huo wawekwa bayana
Umoja wa Mataifa umesema rasilimali lukuki zilizopo kwenye ukanda wa Sahel ni moja ya suluhu mujarabu ya matatizo yanayokabili eneo hilo.
Umoja wa Mataifa umesema rasilimali lukuki zilizopo kwenye ukanda wa Sahel ni moja ya suluhu mujarabu ya matatizo yanayokabili eneo hilo.
Kwa mara ya kwanza, Umoja wa Mataifa unaadhimhisha hii leo siku ya mabunge duniani, ikiwa ni siku pia ambayo Umoja wa Mabunge duniani, IPU ulianzishwa mwaka 1889.
Wakimbizi takribani milioni moja wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar ambao sasa wamekimbilia Bangladesh kutokana na mateso huko nyumbani , jumapili hii watapa ugeni wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameonya juu ya janga linaloendelea huko jimbo la Daraa nchini Syria wakati huu ambapo ghasia zinazidi kuongezeka.
Bahari ya Mediteranea yazidi 'kumeza' watu, manusura wasimulia walivyopata kiwewe.
Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uteguzi wa mabomu ardhini UNMAS, Agnes Marcaillou amesema wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya ongezeko la mabomu ya kutegwa ardhini kwenye maeneo mengi duniani.
Wasaka hifadhi 40,000 wameingia Ulaya kupitia bahari ya Mediteranea mwaka 2018, idadi ambayo ni pungufu mara 6 ikulinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2016, baada ya idadi kufikia kiwango cha juu mwaka 2015..
Ugaidi unasalia kuwa tishio kubwa la maisha ya watu na miundombinu duniani na Umoja wa Mataifa mjini New York unalitambua hilo ndio maana juma hili umeitisha mkutano wa ngazi ya juu uliotoa kipaumbele kwa suala hili.
Hali ya usalama na kibinadamu ikiendelea kuzorota nchini Yemen, hususan mji wa bandari wa Hodeidah, WHO imechukua hatua ili kuhakikisha huduma za afya zinaimarika.
Nchini Yemen kuna nuru sasa ya mazungumzo kati ya pande kinzani. Umoja wa Mataifa umeelezea matumaini hayo wakati huu ambapo tayari chombo hicho kimeruhusiwa kusimamia bandari muhmu ya Hodeidah.