Bado haki za mtoto zinasiginwa, miaka 34 tangu CRC- UNICEF
- Mkataba umepitishwa 1989 lakini hali bado tete
- Haki zinapondwaponda kuanzia kuishi hadi kulindwa
- Ni maombolezo badala ya sherehe
Tarehe 5 Oktoba, kombora lilipiga mgahawa katika kijiji kidogo cha Hroza Mashariki mwa Ukraine, na kuua watu 59 waliohudhuria mapokezi ya mazishi kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu OHCHR lilikuwa moja ya matukio mabaya zaidi kwa raia tangu Februari 2022.
Visa vya kutisha vya ukatili dhidi ya watoto hususan waliofurushwa makwao maeneo mbalimbali duniani vimesababisha viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa kurejelea wito wao wa ulinzi wa watoto na kuhakikisha wakati wowote ule haki zao zinalindwa kwa mujib uwa sheria ya kimataifa, na wakati huo huo watendao uhalifu huo wasikwepe sheria.
Maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wamelaani vkali mashambulio makubwa yaliyofanywa na makombora ya Urusi dhidi ya mji wa Odesa nchini Ukraine, mashambulio ambayo yameharibu majengo kadhaa ya kihistoria.
Wimbi jipya la mashambulizi yanayofanywa na Urusi dhidi ya bandari nchini Ukraine linasababisha madhara makubwa duniani ikiwemo changamoto katika uhakika wa upatikanaji wa chakula hasa katika nchi zinazoendelea.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake makubwa kufuatia kitendo cha Urusi cha sio tu kujiondoa katika Mpango wa kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi bali pia kuondoa hakikisho lake la ulinzi kwenye eneo la majini huko kaskazini magharibi mwa Bahari Nyeusi.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo (Julai 12) leo mjini Geneva, Uswisi ameeleza namna ambavyo Vita ya Urusi dhidi ya Ukraine inaendelea kusababisha ukikukwaji mkubwa wa haki za binadamu alipokuwa kwenye Majadiliano ya Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamezindua mpango wa pamoja kwa ushirikiano na shirika la FSD (Fondation Suisse de Déminage) kusaidia wakulima wadogo na familia za vijijini zilizoathiriwa zaidi na vita huko nchini Ukraine.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Matthew Hollingworth amelaani vikali shambulio lililofanywa na Urusi kwenye eneo la Kherson lililoathirika vibaya na mafuriko ya bwawa la Kakhovka, na kukatili maisha ya mfanyakazi wa ukoaji na kujeruhi wengine.
Milipuko ya magonjwa, changamoto ya afya ya akili na ukosefu wa huduma ni miongoni mwa athari mbaya za kiafya za uharibifu wa bwawa la Kahkovka lililotokea kusini mwa Ukrainia wiki moja iliyopita, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.