Umeme, mabomu ya kutengwa ardhini na uchumi vipewe kipaumbele Ukraine: Griffiths
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Martin Griffiths amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Ukraine na kutaja mambo makuu matatu muhimu ya kupatiwa kipaumbele kuwa ni mosi; kurejesha umeme kwenye makazi, pili kutegua mabomu yaliyoko kwenye makazi ya watu na tatu, ni kuchechemua shughuli za kiuchumi ili maisha yaweze kuendelea na kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia.