Idadi ya wakimbizi wa ndani Ukraine yakaribia milioni 6.5: IOM
Mashambulizi yanayoendelea nchini Ukraine kwa takriban mwezi mmoja sasa yamesababisha zaidi ya watu milioni 6.48 kuwa wakimbizi wa ndani nchini humo.
Mashambulizi yanayoendelea nchini Ukraine kwa takriban mwezi mmoja sasa yamesababisha zaidi ya watu milioni 6.48 kuwa wakimbizi wa ndani nchini humo.
Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, leo amezungumza dhidi ya hali mbaya kuhusu baadhi ya wakimbizi wanaokimbia kuvuka mpaka wa Ukraine, na raia wa nchi ya tatu, kwamba wamekuwa wakikabiliwa na ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine.
Ubaguzi umeendelea kutia sumu kwenye taasisi, miundo ya kijamii na katika maisha ya kila siku, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo wakati wa mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika jijini New York, Marekani juu ya kile kinachoitwa kuwa kichocheo cha kuhalalisha chuki, kupinga utu na kusambaza ghasia.
Katika siku ya 24 ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, na wakati mapigano yakizidi, haswa katika miji ya Mariupol, Sumy, Kharkiv, Chernihiv, Sievierodonetsk na kaskazini mwa Kyiv, mashirika ya kibinadamu yameelezea wasiwasi wao mkubwa juu ya hatima ya raia walionaswa katika miji iliyozingirwa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo tena limekutana kujadili vitisho vya amani na usalama duniani ikijikita zaidi katika uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ambapo Mkuu wa Idara ya siasa kwenye Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo amesema dalili nzuri zilizoonekana wiki hii kufuatia mazungumzo kati ya wawakilishi wa mataifa hayo mawili bado hazijazaa matunda yoyote.
Urusi isitishe operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine, imesema Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki, ICJ katika uamuzi wake iliyotoa leo huko The Hague, nchini Uholanzi.
Iwapo vita vitaendelea Ukraine, mafanikio yote ya kiuchumi yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 18 yatatoweka, huku theluthi moja ya wananchi wakitumbukia kewnye lindi la umaskini katika miezi 12 ijayo, imesema utafiti mpya uliotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP.
Ni wiki mbili sasa tangu Urusi ianzishe mashambulizi yake nchini Ukraine, kitendo hicho kimesambaratisha familia ikiwemo wanaume kulazimika kusalia Ukraine ili kupigana vitani huku familia zao zikilazimika kukimbia maeneo mengine ya taifa hilo au hata nje ya Ukraine.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa mara nyingine tena amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani hii leo na kusema Ukraine inazidi kuteketea mbele ya macho ya dunia na madhara ya vita kwa wanancih hayana kipimo.