‘Tuko nanyi’ Martin Griffiths akielezea mpango wa dharura kwa maafa ya bwawa la Ukraine
Mipango ya kuwasaidia watu wa Ukraine kufuatia uharibifu wa Bwawa la Kakhovka imejikita katika kuokoa watu "hivi sasa", Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, Martin Griffiths ameiambia UN News katika mahojiano yaliyofanyika leo Ijumaa jijini New York, Marekani.