Watu walioondolewa Rafah wafikia 360,000 huku UN ikitoa ombi la dola bil 2.8 kusaidia Gaza na Ukingo wa Magharibi
Takriban watu 360,000 wamekimbia eneo la Rafah katika wiki iliyopita huku kukiwa na mashambulizi yanayoendelea ya wanajeshi wa Israel ambayo yamelemaza uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu na inaaminika yamemuua mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.