Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la moto lalazimisha UNRWA kufunga kwa muda kituo chake Jerusalem Mashariki

Philippe Lazzarini, Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA. (Maktaba)
© UN Photo/Srdjan Slavkovic
Philippe Lazzarini, Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA. (Maktaba)

Shambulio la moto lalazimisha UNRWA kufunga kwa muda kituo chake Jerusalem Mashariki

Amani na Usalama

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limefunga kwa muda makao yake makuu ya Jerusalem Mashariki katika eneo linalokaliwa baada ya shambulio la moto leo Alhamisi kufuatia wiki kadhaa za maandamano.

Katika ujumbe wake kupitia mitandao ya kijamii, Kamishna Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini amesema "wakaazi wa Israeli wamechoma moto mara mbili maeneo haya". 

Wafanyakazi wa UNRWA na wafanyakazi kutoka mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa walikuwa ndani ya jengo wakati huo.

"Mkurugenzi wetu akisaidiana na wafanyakazi wengine walilazimika kuzima moto huo wenyewe kwani ilichukua vifaa vya kuzimia moto vya Israel na polisi muda kabla ya kufika," amesema.

Ameongeza kuwa hili ni tukio la pili la kuogofya katika kipindi cha chini ya wiki moja kufuatia maandamano kama hayo yenye vurugu siku ya Jumanne.

Maendeleo ya kutisha

Ingawa hakukuwa na majeruhi miongoni mwa wafanyakazi wa UNRWA, moto huo ulisababisha uharibifu mkubwa katika maeneo ya nje, amesema, akibainisha kuwa kituo cha petroli na dizeli kiko kwenye misingi ya kuhudumia kundi la magari la shirika hilo.

Umati ulioandamana na watu wenye silaha ulishuhudiwa nje ya jengo hilo la UNRWA wakiimba "choma moto Umoja wa Mataifa," ameongeza.

Ameongeza kuwa "Haya ni maendeleo ya kutisha, kwa mara nyingine tena, maisha ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa yalikuwa hatarini sana."

Maandamano yaligeuka kuwa vurugu

Bwana Lazzarini amesema amechukua uamuzi wa kufunga kituo hicho "hadi usalama ufaao utakaporejeshwa".

Waisraeli wenye itikadi kali wamekuwa wakifanya maandamano nje ya makao ya UNRWA mjini Jerusalem katika muda wa miezi miwili iliyopita "yaliyoitishwa na mwanachama aliyechaguliwa wa manispaa ya Jerusalem."

Amebainisha kuwa maandamano ya Jumanne yamekuwa ya vurugu wakati waandamanaji waliporushia mawe wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo, chini ya uangalizi wa polisi wa Israel.

Unyanyasaji, vitisho na uharibifu

“Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakinyanyaswa na kutishwa mara kwa mara. Kiwanja chetu kimeharibiwa vibaya na kusambaratishwa. Mara kadhaa, Waisraeli wenye msimamo mkali waliwatishia wafanyakazi wetu kwa bunduki,” amesema.

Mkuu huyo wa UNRWA amesisitiza kuwa ni jukumu la Israel kama mamlaka inayokalia kwa mabavu kuhakikisha kuwa wafanyakazi na vifaa vya Umoja wa Mataifa vinalindwa wakati wote.

"Ninatoa wito kwa wale wote ambao wana ushawishi kukomesha mashambulizi haya na kuwawajibisha wale wote waliohusika," amesema akiongeza kuwa “Wahusika wa mashambulizi haya lazima wachunguzwe na waliohusika” wawajibishwe la sivyo kutawekwa kiwango kipya cha hatari.