Nchini Nigeria tamthilia iliyofadhiliwa na WFP, yalenga kuzua gumzo kuhusu mzozo
Mwisho wa mwezi Desemba na Januari wapenda sanaa nchini Nigeria watashuhudia sanaa ya tamthilia kwa jina Bintu iliyotungwa na kuandaliwa kwa ufadhili wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na ukumbi wa maonyesho wa Mosaic.