Ndoto yangu imetimia, nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu- Mtoto Rehema
Hatimaye mtoto Rehema Paul ambaye aliponea chupuchupu kuajiriwa kazi za ndani baada ya mwajiri wake kubaini kuwa umri wake haukuwa unaruhusu kufanya kazi, sasa ameanza masomo katika shule ya msingi Mchikichini, kwenye manispaa ya Morogoro nchini Tanzania.