Neno la Wiki- “Mtambua ndwele ndiye mganga”
Katika Neno la wiki hii Mchambuzi wetu ni mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora ameangazia methali isemayo “Mtambua ndwele ndiye mganga”
Katika Neno la wiki hii Mchambuzi wetu ni mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora ameangazia methali isemayo “Mtambua ndwele ndiye mganga”
Leo katika makala yetu Flora nducha wa Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Pendo Yeredi Daudi Mratibu wa chuo cha Bearfoot kilichoanziswa na serikali ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanawake wa vijijini huko visiwani Zanzibar, mafunzo ambayo yamekuwa mkombozi mkubwa kwao.&
Mlinda amani kutoka Brazili anayehudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya kati MINUSCA, Ijumaa hii anakabidhiwa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya kijeshi kwa mwaka 2019 katika utetezi wa masuala ya jinsia.
Athari za kimbuga Idai kilichoikumba Msumbiji na kwengineko kimeanika hadhari mzigo wa madeni ya siri ambayo hayajalipwa nchini Msumbuji kwa mujibu wa mtalaam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa .
Serikali ya Zanzibar imepiga hatua muhimu katika masuala ya ukombozi wa mwanamke kama ilivyo katika ya ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 , kuhakikisha mwanamke huyo anapata usawa kwa kijinsia, kiuchumi na kijamii.
Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na asasi mbalimbali za kiaraia, pamoja na serikali wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kupitia malengo 17 yaani SDGs.
Wakimbizi Kakuma nchini Kenya wameshukuru na kupongeza mradi wa nishati mbadala unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Kenya, mfuko wa Bill Gates na shirika la Sanivation.
Hatua za haraka lazima zichukuliwe na jumuiya ya kimataifa kukomesha mzunguko wa machafuko ya kijamii na umwagaji damu unaoendelea nchini Mali machafuko ambayo hadi sasa yameshakatili maisha ya watu 160.
Dalili za wazi na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi zinazoongezeka kote duniani , zinatokea leo kwa kila nchi na hakuna aliye na kinga dhidi ya zahma hii na hakuna kisingizio cha kukwepa kuchukua hatua kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anto
Ukosefu wa ajira kwa vijana hususan kusini mwa jangwa la Sahara ni kizingiti kikubwa kwa maendeleo
ya mataifa mengi barani Afrika kwasababu kundi hilo ndiyo nguvu kazi ya kila taifa.