Neno la Wiki- "Msutu"
Leo katika kujifunza Kiswahili mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania , BAKITA Onni Sigalla Mhariri mwandamizi anafafanua maana ya neno "MSUTU"
Leo katika kujifunza Kiswahili mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania , BAKITA Onni Sigalla Mhariri mwandamizi anafafanua maana ya neno "MSUTU"
Zaidi ya nusu ya watoto wakimbizi milioni 7.1 wa umri wa kwenda shule hawaendi shule, ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo imebainisha. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Suala la mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ambayo nchi zinakabiliana nazo kote ulimwenguni. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika uko mstari wa mbele sio tu kuchagiza kuhusu ulinzi wa mazingira lakini pia kushirikiana na nchi kukabiliana na athari hizo.
Wakati hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Venezuela inazidi kuzorota raia zaidi wa Venezuela wanakimbilia mataifa mengine ya Amerika ya Kusini ambapo takriban raia milioni 4 wa Venezuala wameihama nchi yao. Kando na kuwepo hali mbaya ya usalama na ghasia pia kumeshuhudiwa ukosefu wa madawa,
Mwalimu Joseph Gichana akiwa kijana alikuwa na ndoto ya kufanya kazi na Umoja wa Mataifa.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mafunzo ya ufundi cherehani yaliyotolewa na walinda amani wanawake kutoka Tanzania kwa wanawake wakazi wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini yameanza kuleta matumaini na kudhihirisha jukumu la ulinzi wa amani na uwezeshaji wa jamii nchini humo.
Barani Ulaya ugonjwa wa Surua umesalia kuwa tatizo ambapo takwimu mpya zinaonesha kupungua kwa idadi ya mataifa yaliyokuwa yametokomeza ugonjwa huo.
Mkutano wa 7 wa Tokyo kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, TICADVII ukiendelea huko Yokohama nchini Japan, mashirika ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU pamoja na wadau wamezindua mpago wa kuchagiza ajira ya vijana kwenye sekta ya kilimo cha biashara barani humo.
Alipoondoka nchini Burundi akiandamana na dada yake mwaka 2009, msichana Azam Zabimana alikuwa na umri wa miaka 15.