Shule za jamii zaelimisha watoto ukimbizini
Vita vinavyoikumba Syria vimesababisha mamilioni ya watu kukimbia makwao na watoto wengi kuacha shule. Nchini Lebanon ambako kuna zaidi ya wakimbizi Milioni Moja wa Syria, mashirika ya kibinadamu yanahaha kutoa huduma za elimu kwa watoto wasyria 400,000 wenye umri wa kuandikishwa shuleni.