Wimbi kubwa la Tsunami laleta madhara makubwa Indonesia, UN yasema iko tayari kusaidia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa uliosababishwa na wimbi kubwa la tsunami lililopiga maeneo ya pwani ya kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia jana Jumamosi.