Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mashariki ya Kati

Katibu Mkuu wa UN António Guterres akizungumza na wanahabari kwenye kivuko cha Rafah mpakani mwa Misri na Ukanda wa Gaza 20 Oktoba 2023
UN /Eskinder Debebe

Akiwa Rafah Katibu Mkuu wa UN asema shehena ya misaada inayosubiriwa ni mkombozi kwa walioko Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri ametembelea mpaka wa Rafah ambacho ni Kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hizo sasa kuna mashambulizi yanaendelea baina ya Israel na wanamgambo wa Hamas na kusema Umoja wa Mataifa hivi sasa unafanya mazungumzo ya kufafanua vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza.

Sauti
3'1"
Mashambulizi ya makombora dhidi ya Gaza yanaendelea. (Maktaba)
© UNICEF/Eyad El Baba

UDADAVUZI GAZA: Nini kitafuata baada ya mkwamo Barazani?

Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Marekani ikitumia kura turufu. Sasa nini kinafuatia? Rasimu mpya au kikao cha dharura cha Baraza Kuu? 

Sauti
3'51"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Hassan Shoukry Selim mjini Cairo
UN Photo/Eskinder Debebe

Madai halali hayawezi kuhalalisha ugaidi, na ugaidi hauwezi kuhalalisha adhabu ya pamoja: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Cairo Misri  amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje w anchi hiyo Sameh Shoukry na kisha kuzungumza kwa pamoja na na waandishi wa habari akisema yuko ziarani Mashariki ya Kati kuona misaada ya kibinadamu inayohitajika inawasilishwa kwa wahitaji huko Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Rafah. 

Dkt. Ahmed Al Mandhari, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Mediteranea Mashariki
Video ya UN News

Tunahaha kuendelea na huduma za matibabu Gaza- Dkt. Al Mandhari

Mkurugenzi wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Kanda ya Mediterania ya Mashariki, Dk. Ahmed Al Mandhari, amesema jitihada za kuongeza upatikanaji wa vifaa muhimu vya matibabu kwa ajili ya Ukanda wa Gaza zinaendelea, na hatua zaidi zinachukuliwa kuhakikisha kuwa hospitali zinaweza kuendelea kutoa huduma muhimu kwa wagonjwa wakati huu ambapo mashambulizi dhidi ya hospitali na wahudumu wa afya yamedhoofisha utoaji huduma