Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika 5 ya UN yatoa kauli kuhusu misaada iliyoanza kuingia Gaza

Vitongoji vya Gaza vimesambaratishwa kwa mashambulizi kutoka angani
© UNICEF/Mohammad Ajjour
Vitongoji vya Gaza vimesambaratishwa kwa mashambulizi kutoka angani

Mashirika 5 ya UN yatoa kauli kuhusu misaada iliyoanza kuingia Gaza

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la mpango wa maendeleo UNDP, la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, la kuhudumia watoto UNICEF, la mpango wa chakula WFP na la afya duniani WHO leo wametoa tarifa ya pamoja kuhusu  kuhusu msaada wa kibinadamu alianza kuingia Gaza leo.

Taarifa hiyo ya mashirika matamo inasema “Msaada ulioingia Gaza ingawa ni mdogo unasaidia kuokoa maisha kwa raia, lakini hautoshi na ni mwanzo mdogo tu misaada zaidi inahitajika kuingizwa Gaza.

Msaada huo ni kutoka Hilali Nyekundu ya Misri na Umoja wa Mataifa na ulikuwa umesheheni katika malori 20.

Taarifa hiyo ya pamoja imesema msaada huu ni "njia ya kuokoa maisha kwa mamia ya maelfu ya raia  wengi wao wakiwa wanawake na watoto ambao wamekatishiwa maji, chakula, dawa, mafuta na vifaa vingine vya kimsingi.”

Msaada huo hautoshi

Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yameonyesha kuwa msaada huu hautoshi, na kusema kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 huko Gaza wanahitaji misaada ya kibinadamu, na kwamba watoto, wanawake wajawazito na wazee wanasalia kuwa makundi yaliyo hatarini zaidi. 

Ni vyema kutambua kwamba watoto wanawakilisha karibu nusu ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. Yamesema mashirika hayo.

Pamoja na miundombinu mingi ya raia wa Gaza kuharibiwa au kusambaratishwa  wakati wa karibu wiki mbili za mashambulizi ya mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na makazi, vituo vya afya, mifumo ya maji, mifumo ya usafi wa mazingira na umeme, mashirika hayo yamesema "muda unasonga kabla ya vifo kuongezeka kwa kasi kutokana na milipuko ya magonjwa na uwezo mdogo wa huduma za afya."

Mashirika hayo yamesisitiza kwamba “Ni vyema kutambua kwamba karibu theluthi moja ya wakazi wa Palestina walikumbwa na uhaba wa chakula kabla hata ya mzozo huu hwa sasa kuanza huko Gaza.

Mashirika hayo matano ya Umoja wa Mataifa yametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kwa ajili ya masuala ya kibinadamu na kuhakikisha fursa ya upatikanaji wa misaada ya haraka na usiozuiliwa katika eneo lote la Ukanda wa Gaza, ili wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu waweze kuwafikia raia wote wanaohitaji, kuokoa maisha na kuzuia mateso zaidi ya binadamu.

Pia wamesisitiza haja ya mtiririko wa misaada ya kibinadamu kuendelea na kuwa endelevu.