Sam Aderubo anayeleta 'utamu' kwa jamii yake kaskazini mwa Uganda
Sam Aderubo alianzisha kampuni yake, Honey Pride, huko Arua, kaskazini mwa Uganda, ili kuleta matokeo chanya kwa jamii yake. Kwa msaada kutoka kwa Umoja wa Mataifa, biashara inashamiri, ikitoa kazi kwa mamia ya wafugaji nyuki wa ndani, ambao wengi wao ni wanawake na vijana waliotengwa.