Tushikamane kwa vitendo kupinga ukatili wa kijinsia - Mwanariadha
Violah Cheptoo au Violah Lagat ni maarufu sana sio tu nchini Kenya bali pia nje ya taifa hilo kutokana na umaarufu wake kwenye mbio za nyika au marathoni. Lakini zaidi ya hivyo, Viola anatambulika pia nje ya michezo kuwa mpeperushaji wa bendera ya kupinga ukatili wa kijinsia.