Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN News

Ulemavu sio kulemaa tunachotaka ni kujumuishwa: Mbunge Mollel

Siku hii ya kimataifa ya watu wenye ulemavu inapoadhimishwa kote duniani watu wenye ulemavu wamekuwa wakipaza sauti zao kila kona kwamba ulemavu sio kulemaa wanachohitaji ni ujumuishwashi na miundombinu Rafiki itakayowawezesha kushiriki katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu kama wengine.

Miongoni mwa watu hao ni mbunge Amina Mollel kutoka nchini Tanzania,  yeye mwenyewe ni mlemavu na anawakilisha watu wenye ulemavu wa taifa hilo bungeni, akizungumza nami kwa njia ya simu kutoka mjini Arusha amesisitiza nafasi ya wenye ulemavu katika ujumbe wake.

Sauti
5'35"