Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Meja Asia Hussein

TANZBATT 6 wakabidhiwa jukumu la ulinzi wa amani wa UN nchini CAR

Kikosi cha 5 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANZBATT 5 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, kimekamilisha muda wake  na kukipisha kikosi kingine cha 6 nacho kutoka Tanzania, TANZBATT 6 ambacho kitaendeleza jukumu hilo. Kutoka Berberat, Captain Mwijage Inyoma ni Afisa Habari wa TANZBATT 06 ametuandalia taarifa hii. 

Sauti
2'35"
IOM/Gema Cortes

Tusiwabague wahamiaji, tuwasaidie: IOM

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wahamiaji itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki Desemba 18 shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limemtaka kila mtu kutafakari je muhamiaji ni nani? Mchango wa wahamiaji na na endapo hapa duniani kuna mtu yeyote ambaye hajawahi kufikiria kuondoka alipo na kwenda kusaka mustakhbali bora kwani hii itasaidia kutambua sababu ya uhamiaji na mchango wao katika jamii wanakokwenda.

Natts 

Sauti
2'29"
TANZBATT 7/Ibrahim Mayambua

Walinda amani wa UN na wananchi wakishirikiana amani itapatika DRC

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wameendelea kuhamasishana kuimarisha ushirikiano kati yao ili kufikia lengo kuu la kuleta amani nchini humo. Anayetuletea taarifa hii kwa kina ni Kapteni Denisia Lihaya ambaye ni Afisa Habari wa Kikundi cha 9 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT 9 wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB na kile cha utayari QRF chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO. 

Sauti
1'57"
Picha: UNHCR Kenya

Tatizo la muda mrefu la kutokuwa na utaifa kwa watu wa jamii ya Pemba wanaoishi nchini Kenya latatuliwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepongeza hatua zinazochukuliwa na serikali ya Kenya kutatua tatizo la muda mrefu la kutokuwa na utaifa kwa watu wa jamii ya Pemba wanaoishi nchini humo.

Kwa mujibu wa UNHCR wakati wa maadhimisho ya 59 ya siku ya Jamhuri wiki hii nchini Kenya Rais Willim Ruto alitangaza kwamba serikali itaanza mipango ya mkakati wa kuwatambua watu wa jamii ya Pemba kama rai awa Kenya. 

Sauti
2'48"
© UNICEF/Anwar Al-Haj

UNICEF linahofia kwamba zaidi ya watoto 11,000 wameuawa au kujeruhiwa Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto zaidi ya 11,000 nchini Yemn wameuawa au kujeruhiwa hadi kufikia sasa ikiwa ni sawa na wastani wa watoto 4 kwa siku tangu kushika kasi kwa machafuko nchini humo mwaka 2015. 

Shirika hilo limesema linahofia kwamba idadi kamili ni kubwa zaidi kwani hizi ni takwimu tu za matukio yaliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa.

Sauti
3'55"
CDC/Alissa Eckert, James Archer

Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono umeonesha ukinzani kwa dawa ya kumeza: WHO

Utafiti mpya wa kisayansi uliofanyika kwa muda wa miaka sita umebaini kuna viwango vya juu vya usugu wa dawa dhidi ya vimelea au bakteria vinavyosababisha maambukizi kwenye mfumo wa damu yanayoweza kuhatarisha halikadhalika ongezeko la usugu wa tiba dhidi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa yaliyozoeleka kwenye jamii. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema hayo katika taarifa iliyotolewa leo jijini Geneva Uswisi.

Audio Duration
3'10"
© UNICEF/Mulugaeta Ayene

Jamii katika maeneo ya kusini na kaskazini mashariki mwa Ethiopia bado wanateseka na ukame mbaya zaidi: UNICEF Ethiopia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly akiambatana na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Ethiopia, Gianfranco Rotigliano wametembelea eneo la Afar, nchini Ethiopia kujionea athari za ukame kwa watoto na familia na kutathimini hatua za dharura zizazochukuliwa na UNICEF ambapo Uingereza ni mdau muhimu kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na muhisani. 

Sauti
2'12"
©UNICEF/Benekire

Mama akutanishwa na watoto wake baada ya kutenganishwa kufuatia mashambulizi: UNICEF/CAJED

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa kushirikiana na wadau wake kama shirika lisilo la kiserikali la CAJED (CONCERT D’ACTIONS POUR JEUNES ET ENFANTS DÉFAVORISÉS), wanaendelea na huduma kadhaa muhimu za ulinzi kwa watoto ambazo ni pamoja na utambulisho, matunzo na kuwaunganisha watoto na familia zao.  T

‘’Mapigano yalikuwa yameanza tukiwa shambani. Binti yangu na wengine walikimbia. Walipofika Goma, walipotea njia.” 

Sauti
2'32"
© UNHCR/Charlotte Hallqvist

Mapigano Upper Nile yasababisha wakimbizi wengi wahame makwao nchini Sudan Kusini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ambayo umesababisha takriban watu 20,000 kuyahama makazi yao tangu mwezi Agosti, baadhi yao wakilazimika kukimbia hadi mara nne ili kuokoa maisha yao huku mzozo huo ukiendelea. 

Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis na Juba Sudan takriban watu 3,000 tayari wamekimbilia nchi jirani ya Sudan, na hivyo kuzidisha mzozo wa wakimbizi wa Sudan Kusini, ambao ndio mkubwa zaidi barani Afrika. 

Sauti
2'57"