Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© UNICEF/Karin Schermbrucker

Mtandao thabiti wa Intaneti kutaimarisha ukuaji jumuishi na endelevu Afrika. UN

Nchi za Afrika zimechagizwa kuwekeza katika kujenga mnepo wa miundombinu thabiti ya ya mtandao wa intaneti ili kutumia fursa za kidijitali na kuharakisha mageuzi ya kijamii na kiuchumi barani humo.

Hayo yameelezwa na viongozi wa kimataifa wanaohudhuria kongamano la 17 la udhibiti wa mtandao IGF 2022 linalofanyika Addis Ababa, Ethiopia, wakisisitiza umuhimu wa teknolojia ya kidijitali kama zana za kuimarisha maendeleo kote barani Afrika. 

Sauti
3'39"
© UNICEF/Uganda

UNICEF yawezesha wanafunzi waliokuwa karantini Uganda kufanya mitihani

Nchini Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limewezesha wanafunzi wa shule moja ya msingi nchini humo kufanya mtihani wa kuhitimu shule ya msingi baada ya shule hiyo kulazimika kufungwa na wanafunzi kuwekwa karantini kufuatia mwanafunzi mmoja kupata maambukizi ya Ebola, mlipuko uliotangazwa mwezi SEptemba mwaka huu.

Tarehe 20 mwezi Septemba mwaka huu wa 2022, Wizara  ya Afya nchini Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola, mlipuko ambao ulihatarisha kuvuruga mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa wanafunzi wa darasa la saba. 

Sauti
2'6"
©UNICEF/Nzaramba

Kutoka Cyangugu Rwanda hadi kuwa mwamuzi fainali za kombe la dunia, Qatar- Simulizi ya Salima

Michuano ya Kombe la Dunia inaendelea nchini Qatar huko Mashariki ya Kati. Mmoja wa watu wanaong’ara katika michuano hii ni Mchechemuzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Rwanda, Salima Mukansanga, ambaye ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa mwamuzi au refarii katika Kombe la Dunia. Aliingiaje katika tasnia hii ya mpira wa miguu? UNICEF Rwanda ilizungumza naye kabla hajasafiri kwenda Qatar na hapa Anold Kayanda anaeleza kwa lugha ya Kiswahili kilichozungumzwa. 

Sauti
2'39"
© Harun Tulunay

Ugonjwa wa Monkyepox au Ndui ya Nyani wabadilishwa jina na kuwa MPOX

Baada ya mfululizo wa mashauriano na wataalamu wa kimataifa, hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO litaanza kutumia jina MPOX badala ya Monkeypox au homa ya Ndui ya Nyani kufuatia mapendekezo ya kubadilishwa kwa jina hilo kwa maelezo ya kwamba lilikuwa linasababisha mambo kadhaa ikiwemo unyanyapaa. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Sauti
2'24"
UN Women

Wanawake wajumuika kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali. Dadaab Kenya 

Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na wadau wanajengea uwezo wajenzi wa amani mashinani hata kwenye maeneo yenye changamoto kama vile kambi ya wakimbizi ya Daadab kwenye kaunti ya Garissa nchini humo kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali.  

Sauti
2'15"
© UNICEF/Odelyn Joseph

Hali halisi hususan ya watoto katika moja ya kituo cha matibabu ya kipiondupindu cha UNICEF nchini Haiti

Ikikaribia miezi miwili tangu kuzuka kwa mlipuko wa kipindupindu nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba takriban asilimia 40 ya ongezeko la idadi ya wagonjwa ni watoto na hatua zaidi zinahitajika ili kuwanusuru.

Kwa mujibu wa UNICEF tangu kuzuka kwa mlipuko wa kipindupindi nchini Haiti wagonjwa 9 kati ya 10 waliothibitishwa wako katika maeneo ambayo yana mgogoro mkubwa wa lishe nchini humo. 

Sauti
2'12"
© UNICEF/Malawi

Jamii wawezeshwa kupunguza umaskini, kukabili utapiamlo halikadhalika kuondokana na utoro shuleni: UNICEF Malawi

Nchini Malawi,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF kwa msaada kutoka kwa wadau wake wa maendeleo linatekeleza mradi wa kupatia fedha jamii au MSCTP kwa ajili ya kupunguza umaskini, kukabili utapiamlo halikadhalika kuondokana na utoro shuleni utokanao na wazazi kushindwa kulipa karo. 

Nats…

Sauti
2'36"
UN Women/Fatma Elzahraa Yassin

Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni moja ya ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu duniani: UN Women/UNODC

Ripoti ya utafiti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC inaonyesha kuwa wanawake na wasichana ndio walio katika hatari kubwa ya kuuawa majumbani, ikionyesha kuwa kwa wastani zaidi ya wanawake au wasichana watano waliuawa kila saa na wenzi wao au jamaa wa familia kwa mwaka 2021.

Sauti
3'33"
UNICEF VIDEO

Mradi wa vyoo unaofadhiliwa na UNICEF wasaidia kupunguza kipindupindu

Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wadau wake wameanzisha mradi wakujenga vyoo uitwao Fresh Life lengo ni kusaidia kuhakikisha wananchi wanapata ufikiaji wa vyoo safi, salama pamoja na usafi wa mazingira na matokeo yake ni kupunguza ugonjwa wa Kipindipindu kwa kiingereza Cholera.

Tayari mradi huo umewanufaisha zaidi wa wakazi 120,000 wa mijini akiwemo mama huyu mwenye nyumba yenye wapangaji zaidi ya 32 ambaye ameishi bila choo kwa zaidi ya miaka 10. Anaanza kwa kijitambulisha.....

Sauti
2'16"
Unsplash/Roberto Carlos Roman Don

Sekta ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha uhakika wa chakula: FAO

Ikiwa leo ni siku ya uvuvi duniani imeelezwa kuwa sekta ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha uhakika wa chakula na inasaidia mtu 1 kati ya 10 duniani kote. Kwa kutambua mchango wake wito umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuboresha miasha ya mamilioni ya wanawake kwa wanaume wanaofanyakazi katika sekta hii kwa kuhakikisha haki zao za binadamu zinatimizwa.  

Sauti
2'58"