Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© UNICEF/ Thoko Chikondi

Nchini Malawi, ubunifu wa UNICEF kusambaza chanjo ya Covid-19 mtaa kwa mtaa wazaa matunda

Mnyumbuliko wa hivi karibuni wa virusi vya Corona vinavyosababisha Covid-19, Omicron ukiwa umesambaa ulimwenguni kote, ukosefu wa usawa wa chanjo unaweka baadhi ya watu hatarini zaidi kuruhusu minyumbuliko kubadilika na kuathiri wanadamu wengine. Afrika ina idadi ya chini zaidi ya watu waliochanjwa dhidi ya COVID-19 duniani lakini nchini Malawi mradi bunifu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kusambaza chanjo kwa njia ya gari unaongeza upatikanaji wa chanjo na imani ya chanjo miongoni mwa wanawake wajawazito katika jamii za vijijini.

Sauti
1'57"
UNMISS/Video Still

Lt. Jenerali Tinaikar - Walinda amani wanawake wanafanya wanafanya kazi nzuri

Luteni Jenerali Shailesh Tinaikar raia wa India ambaye anastaafu wadhifa wake kama Kamanda wa Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS amewashukuru askari walinda amani waliokuwa chini yake hususani wanawake ambao anasema wanafanya kazi katika mazingira yenye changamoto zaidi. John Kibego anaeleza zaidi.

Ni Luteni Jenerali Shailesh Tinaikar akikagua gwaride la wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliosimama kikakamavu.  

Sauti
2'31"
© FAO/Alessio Romenzi

Wakulima wa Afghanistan wapatiwa mbegu bora za kuhimili ukame

Msimu wa upanzi wakati wa majira ya chipukizi ukiwa unakaribia huko nchiin Afghanistan, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limepatia wakulima mgao wa mbegu bora za ngano ili kuepusha njaa ilIyowakumba mwaka jana kutokana na kuchelewa kupanda mbegu bora wakati wa msimu wa baridi kali. Taarifa zaidi na Anold Kayanda.

Mgao wa mbegu bora za mahindi umefanyika kando sambamba na mafunzo ya kilimo bora huko Damani katika jimbo la Kandahar nchini Afghanistan.

Sauti
1'41"
© UNOCHA

Mkimbizi wa Syria - Msimu wa baridi ni kama tunaishi katika jokofu

Familia za wakimbizi wa ndani pamoja na zile zilizowakaribisha wakimbizi hao katika ukanda wa mashariki ya kati kwa sasa zinakabiliana na baridi kali kutokana na kuanguka kwa theluji wakati huu wanaishi kwenye mahema.Taarifa ya MINUSCA inayosomwa studio na Happiness Palangyo wa radio washirika Radio Uhai FM inafafanua zaidi. 

Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inaonesha madhila wanayokumbana nayo wakimbizi wa ndani wa Iraq, Syria, Jordan.

Sauti
2'39"
© UNHCR/Haidar Darwish

UNHCR yaonesha namna COVID-19 ni ‘mwiba’ kwa wakimbizi na raia nchini Lebanon

Nchini Lebanon, athari za kiuchumi zinazosababishwa na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19, zinaacha raia wa Lebanon pamoja na wakimbizi kutoka Syria wakihaka kujikimu huku baridi kali nayo na njaa vikikosa majawabu.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linasema, mwaka huu wa 2022, hali ni tete zaidi kwa kuwa Lebanon nayo nyenyewe imetwama kwenye janga la kiuchumi, hali iliyosababisha na wakimbizi nao kuwa katika hali ya umaskini uliokithiri. 

Sauti
1'43"
© UNRWA 2021/Mohamed Hinnawi

Mafunzo ya UNRWA  yafungua macho si tu wanafunzi bali pia walimu katika ukanda wa Gaza

Programu ya kufundisha masuala ya haki za binadamu katika shule za watoto wakimbizi wa kipalestina katika ukanda wa Gaza,  imesaidia siyo tu wanafunzi kutambua haki zao bali pia walimu ambao wanawafundisha na hivyo kusaidia katika kusongesha amani kwenye eneo ambalo hugubikwa na migogoro. Taarifa iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA inasomwa hapa studio na Happiness Pallangyo wa Radio washirika Radio Uhai FM ya Tabora Tanzania. 

Sauti
2'24"
Meja Asia Hussein

Wakazi wa Mambéré-Kadéï wapokea kwa furaha msaada wa maji kutoka walinda amani kutoka Tanzania, TANBATT-5

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBATT-5 kwenye ujumbe wa umoja huo unaolinda amani nchini humo MINUSCA, kando mwa jukumu lao la ulinzi wa raia wamechukua jukumu la kusambaza huduma za maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo  ambako wanalinda amani kama njia mojawapo ya kuimarisha ulinzi wa raia. Kwa kina basi kuhusu taarifa hii tuungane na Meja Asia Hussein, Afisa habari wa kikosi cha 5 cha Tanzania nchini CAR, TANBATT-5.

Sauti
1'32"
© FAO/Lena Gubler

IFAD yasaidia wanawake wa kisiwani Sumar Ufilipino kujikomboa kiuchumi 

Mradi wa samaki unaofadhiliwa na Mfuko wa  Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo duniani FAO na Serikali ya Ufilipino, umekuwa mkombozi kwa wakina mama ambao hapo awali walikuwa hawana shughuli ya kuwaingizia kipato na sasa wanawake hao, wamejiinua kiuchumi kwa kutumia mbinu walizojifunza enzi za utotoni pamoja na utaalamu wa kisasa waliopatiwa.

 

Asubuhi ya kupendeza yenye pilika pilika kwa wafanyabiashara wa soko la Guiyang nchini Ufilipino, katika kisiwa cha Sumar kilichoko mashariki mwa nchi hiyo.

Sauti
3'33"