Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN/ Evan Schneider

Ubaguzi wa kimfumo dhidi ya watu wenye asili ya Afrika bado kutokomezwa

Hatua za kutokomeza ubaguzi wa kimfumo dhidi ya watu wenye asili  ya Afrika zinatekelezwa vipande vipande licha ya serikali mbalimbali duniani kutangaza hatua za kumaliza kitendo hicho dhalimu, imesema ripoti ya Umoja wa Mataifa itakayowasilishwa mbele ya Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu Jumatatu ijayo. Leah Mushi na maelezo Zaidi.

Sauti
2'5"
© UNICEF/Kinny Siakachoma

Ushiriki mapema wa baba na mama kwenye malezi ya mtoto waongeza uelewa wa mtoto

Nchini Zambia wakazi wa kijiij cha Kholowa wilaya ya Katete jimbo la Mashariki wameanza kuona manufaa ya mradi wa maendeleo ya mapema ya mtoto, ECD unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mradi ambao alianza mwaka 2018 na unashirikisha baba na mama katika malezi ya mtoto tangu akiwa tumboni mwa mama yake hadi anapozaliwa na anapoendelea kukua. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. 

Nyumbani kwa Posilio Phiri akisema UNICEF ilianza kwa kutufundisha jinsi ya kucheza na mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. 

Sauti
2'6"
FAO Tanzania

Mradi wa zaidi ya dola milioni 9 kuimarisha mimea na usalama wa chakula wazinduliwa na FAO Tanzania

Katika kutekeleza lengo namba 15 la  Maendeleo  endelevu kuhusu kuimarisha uhai wa viumbe vya nchi kavu Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa kushirikiana na  Muungano wa Ulaya, (EU) limezindua  mradi wa kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea na usalama wa chakula nchini Tanzania.

Afisa Afya ya Mimea kutoka FAO, Mushobozi Baithani anasema lengo la mradi huo ni kuboresha sekta ya mimea na mazao pamoja na kutatua changamoto kwa wafanyabiashara.

Sauti
3'1"
© WFP

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuangazia zaidi mwelekeo wa mkataba wa amani Sudan Kusini

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuangazia zaidi na kwa mwelekeo wa mkataba wa amani Sudan Kusini pamoja na ongezeko la ghasia miongoni mwa jamii nchini kote Sudan Kusini, wameonya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini humo baada ya kuhitimisha ziara yao jijini New York, Marekani ambako wamepata fursa ya kuzungumza na maafisa mbalimbali. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Sauti
2'18"
© UNICEF/Frank Dejongh

Kipindi cha mpito Burkina Faso tunachukua hatua kurejesha utulivu- Rais Damiba

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77 ukiwa umeingia siku ya nne hii leo, Rais Paul Damiba wa Burkina Faso amesema tayari wamejiwekea mpango mkakati wa kurejesha utulivu nchini mwake wakati huu ambapo anaongoza serikali ya mpito kuanzia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Januari mwaka huu.

Rais Damiba amesema hali ya usalama Burkina Faso alianza kuzorota mwaka 2015 na kilele kufikia mwaka 2020/2021 hali iliyosababisha changamoto kama vile ukimbizi wa ndani, kutwama kwa shughuli za kiuchumi.

Sauti
1'45"
UN News/ Thelma Mwadzaya

Baada ya kunusurika kuozwa kisa ukame, mtoto 'Carol' sasa aomba asaidiwe aende shule

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto wengi na hususan wa kike katika jamii zilizoathirika na ukame nchini Kenya ikiwemo Turkana wako katika hatari  hasa ya kuozwa mapema kwa sababu familia nyingi zinahaha kuweka mlo mezani na suluhu ya karibu wanayoiona ni kuoza binti zao mapema ili kujikimu. Sasa shirika hilo linashirikiana na mamlaka za huduma ya ulinzi kwa watoto katika maeneo yaliyoathirika ili kuwalinda dhidi ya ajira ndoa za utotoni. Mary Kabora na maelezo zaidi.

Sauti
3'35"
Public domain

Kando ya UNGA77, viongozi wa nchi wakutana kujadili magonjwa yasiyoambukiza

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwengiuni WHO leo kandoni mwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini Newy York Marekani limezindua ripoti mpya inayowataka viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs ambayo hukatili Maisha ya watu milioni 17 kila mwaka. Leah Mushi na taarifa Zaidi

Sauti
2'22"
Gibson Kawago

Kiu ya kutafuta nishati salama nyumbani ilisababisha kubuni matumizi ya betri chakavu kutengeneza nishati

Kijana Gibson Kawago kutoka Tanzania ambaye ni miongoni mwa vijana 17 walioteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa viongozi vijana wa kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema atatumia kipindi cha miaka miwili cha nafasi hiyo kusongesha hatua kwa tabianchi ikiwemo kutumia ugunduzi wake kuchakata betri chakavu za kompyuta kutengeneza betri za kuzalisha umeme katika kulinda na kuhifadhi mazingira.  

Nina furaha sana kuteuliwa na nitakuwa balozi mwema 

Sauti
3'23"