Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN News

Wavuvi wanawake Kigoma wapata mtandao wao, shukrani kwa FAO

Katika kutekeleza lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu ajira za staha na ukuaji kiuchumi sambamba na namba 5 la usawa wa kijinsia, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani FAO nchini Tanzania,  limezindua tawi la tatu la Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika. Devotha Songorwa wa Radio Washirika KIDS Time  FM ya Morogoro nchini Tanzania ameshuhudia uzinduzi na kuandaa taarifa hii.

Sauti
4'19"
Picha ya UNICEF/Alessio Romenzi

UNHCR yataka usaidizi zaidi wa ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji

Pengo la huduma za ulinzi safari latumbukiza wakimbizi mikononi mwa wasafirishaji haramu

Kuelekea sikuya kimataifa dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu kesoh Julai 30, shirika la umoja wa Mataifa la wakimbizi duniani, UNHCR imesema ukosefu wa huduma za ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji wanaofanya safari hatarishi kutoka ukanda wa Sahel na Pembe ya Afrika kwenda Afrika Kaskazini na kisha Ulaya, kunawatumbukiza katika hatari ya mikono ya wasafirishaji haramu. Leah Mushi na taarifa zaidi.

Sauti
2'23"
UN News

Sintofahamu kubwa juu ya mwelekeo wa uchumi duniani - IMF

Ripoti ya hali ya uchumi kwa robo ya pili ya mwaka huu wa fedha ambao ni mwezi Aprili hadi Juni ambayo imetolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imesema matarajio ya ukuaji wa uchumi duniani yanazidi kukumbwa na kiza na yanakosa uhakika na kwamba matumaini ya uchumi kukwamuka mwaka 2021 yanazidi kuyoyoma mwaka huu wa 2022. Taarifa iliyoandaliwa hapa studio inasomwa na Evarist Mapesa wa redio washirika SAUT FM

Sauti
2'34"
UN/Boybe Malenga

Wahusika wa vurugu dhidi ya UN kukumbwa na mkono wa sheria- DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imesihi utulivu miongoni mwa wananchi baada ya maandamano na uvamizi dhidi ya vituo vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kwenye miji ya Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini, tukio ambalo hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka mamlaka zichunguze na sheria ichukue mkondo wake. Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ana taarifa zaidi.

Sauti
3'22"
© UNICEF/Frank Dejongh

Dola 17 kwa mwezi kutoka UNICEF zabadilisha maisha ya familia Kajiado

Wakati Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu tarehe 9 mwezi ujao wa Agosti, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo linatoa wito kwa serikali itakayoingia madarakani ipatie kipaumbele hifadhi ya jamii ikiwemo kupatia fedha familia zilizo hatarini kama njia mojawapo ya kupunguza umaskini. UNICEF inatoa wito huo wakati huu ambapo mradi wake wa majaribio kupatia fedha famiilia maskini zenye watoto umeanza kuzaa matunda kama anavyoelezea Anold Kayanda katika taarifa hii.

Sauti
2'31"
© UNICEF/Scott Moncrieff

Kuteka maji kisimani ni moja ya sababu za watu kuzama majini- WHO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia kuzama majini duniani Shirika la Umoja wa Afya duniani WHO limetoa wito kwa watu wote duniani kuongeza juhudi za kupunguza vifo vitokanavyo na watu kuzama kwenye maji, huku likitoa mapendekezo sita ya kusaidia kupunguza vifo na ajali zinazosababishwa na watu kuzama majini duniani kote. Leah Mushi na maelezo zaidi.

Sauti
2'53"
© FAO/Petterik Wiggers

"Baho Neza" au Ishi Vizuri wastawisha jamii nchini Rwanda

Kupitia Mpango wa UN Moja ambapo mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa hushirikiana kutekeleza miradi, huko nchini Rwanda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linafanya kazi bega kwa bega na mashirika dada likiwemo la Mpango wa Chakula Duniani, WFP na la Chakula na Kilimo, FAO kutekeleza mradi wa Baho Neza au Ishi Vizuri kwa kutumia maafisa ustawi wa jamii wenyeji wanaojitolea. Anold Kayanda ameangazia mradi huo unaoenda vizuri na hii ni taarifa yake.  

Sauti
2'41"
Umoja wa Mataifa

Ukraine na Urusi zatia saini makubaliano ya kuruhusu usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia bahari nyeusi

Hatimaye makubaliano ya kuruhusu meli zilizojaa shehena za nafaka kutoka nchini Ukraine zipite kwenye baharí nyeusi yamefikiwa hii leo huko Instanbul Uturuki baina ya Ukraine na Urusi yakishuhudiwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amesema makubaliano hayo yameleta nuru kwa ulimwengu kupata ahueni kwenye be iza mazao ya chakula katika soko la kimataifa.

Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

Sauti
3'19"
UNMISS/Nektarios Markogiannis

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa waendesha doria huko Tambura kwa lengo la kulinda raia

Kufuatia mauaji ya raia huko jimboni Tambura nchini Sudan Kusini katika kipindi cha miezi sita iliyopita na zaidi ya wakazi elfu 80 kulazimika kukimbia makazi yao, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS unaendesha doria za mara kwa mara jimboni hapo huku ukitoa ulinzi kwa maelfu ya raia walioyakimbia makazi yao. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

Video ya UNMISS ikionesha watoto wakicheza mtaani kwa furaha, huku wanajamii wengine wakiendelea na shughuli za kila siku kama vile kubeba kuni kwa ajili ya kuuza na kutumia nyumbani.

Sauti
3'7"
© WFP/Martin Karimi

COVID-19 na Ukraine vimetulazimu tupunguze ukubwa wa chapati- Prince 

Athari za kibiashara kutokana na COVID-19 pamoja na vita nchini Ukraine zinaendelea kusambaa duniani na zimebisha hodi hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi ambako ,mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amelazimika kupunguza ukubwa wa chapati ili angalau aweze kuendelea kutoa huduma hiyo pendwa kwa wakimbizi na wakati huo huo apate angalau faida kidodo ili akidhi mahitaji yake na aweze kujitegemea. Taarifa ya Happiness Pallangyo wa Radio WAshirika Uhai FM kutoka mkoani Tabora nchini Tanzania inafafanua zaidi.

 

Sauti
2'42"