Cameroon yatengewa dola milioni 6 kutoka CERF
Taarifa iliyotolewa na mfuko mkuu wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF mjini Yaounde, Cameroon, inaelezwa kuwa Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ameidhinisha kutengwa kwa Dola za Marekani milioni 6 kutoka katika mfuko huo ili kutoa msaada wa kuokoa maisha na ulinzi kwa watu walioathiriwa na majanga ya kibinadamu nchini Cameroon.