Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ziara ya Katibu Mkuu katika Ikulu ya Marekani

Ijumanne KM Ban Ki-Moon alizuru Ikulu ya Marekani mjini Washington DC na kufanya mkutano rasmi, wa awali, na Raisi wa Marekani George Bush. Ziara hiyo ilihusika na hishima za kidiplomasia kwa Serekali Mwenyeji wa UM, yaani Serekali ya Marekani, ziara ambayo KM mpya anawajibika kuikamilisha.~

Baraza la Usalama lapendekeza kuchukuliwe hatua za dharura katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Januari, Balozi Vitaly Churkin wa Shirikisho la Urusi aliwaambia waandishi habari waliopo Makao Makuu ya UM kwamba wajumbe wa mataifa 15 katika Baraza hilo walikubaliana kupendekeza kwa KM Ban Ki-moon atayarishe haraka tume ya utangulizi itakayozuru Chad na pia Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mashauriano na serekali za mataifa haya mawili. Baadaye KM alitakiwa atayarishe ripoti ya mapema itakaousaidia UM kuandaa operesheni za ulinzi wa amani katika eneo lao.

Kumbukumbu za mkutano wa awali wa KM mpya na vyombo vya habari

KM Ban Ki-moon alifanyisha mkutano rasmi wa kwanza na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa waliopo Makao Makuu ya UM mjini New York mnamo Alkhamisi ya tarehe 11 Januari 2007. KM Ban aliwafafanulia ratiba ya masuala aliyokabiliana nayo siku 10 baada ya kuchukua madaraka ya kuongoza taasisi hii muhimu ya kimataifa.

UM waashiria mwelekeo wa uchumi wa dunia kwa 2007

Katika kila mwanzo wa mwaka, UM huwasilisha ripoti maalumu kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya uchumi duniani, ripoti ambayo huandaliwa na idara mbalimbali za UM, ikijumuisha Idara Inayohusika na Masuala ya Kiuchumi na Jamii (DESA), Shirika la UM kuhusu Maendeleo ya Uchumi na Biashara (UNCTAD) pamoja na kamisheni tano za kikanda zinazoshughulikia huduma za uchumi, yaani Kamisheni ya ECA, kwa Afrika, ECE, kwa Mataifa ya Ulaya, ECLAC, kwa Amerika ya Latina na Maeneo ya Karibiani, ESCAP, kwa mataifa ya Asia na Pasifiki na vile vile Kamisheni ya ESCWA, inayohusika na maendeleo ya Asia ya Magharibi. ~~