Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Huduma za UM kusaidia mamia elfu ya waathiriwa wa mafuriko Kenya

Mashirika ya UM yanayohusika na miradi ya chakula duniani (WFP), wahamiaji (UNHCR), na pia mfuko wa maendeleo ya watoto (UNICEF) yalijumuika nchini Kenya wiki hii kuongoza operesheni za kugawa misaada ya kiutu kwa mamia elfu ya wahamiaji wa Usomali walioajikuta kunaswa na mafuriko yaliozuka kwenye zile kambi walizokuwa wakiishi kaskazini-mashariki ya Kenya.

Kenya kuchachamaa kutunza mazingira dhidi ya uharibifu wa hali ya hewa

KM wa UM Kofi Annan alipohutubia kikao cha wawakilishi wa Hadhi ya Juu kwenye Mkutano Mkuu juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa alisisitiza ya kuwa ni lengo la jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwepo maelewano mazuri miongoni ya watu, na vile vile kuhakikisha kuna mlingano wa kimaumbile kati ya wanadamu na mazingira asilia, mazingira ambayo uhai wetu huyategemea kumudu maisha.

UNHCR kuhudumia maelfu ya wahamiaji wa Usomali walioathiriwa na mafuriko nchini Kenya

Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripotiwa kushiriki hivi sasa kwenye shughuli kuhudumia misaada ya kihali kwa maelfu ya Wasomali walioathirika na maafa ya mvua kali zilizojiri karibuni katika eneo la kaskazini-mashariki ya Kenya, hususan katika zile kambi za wahamiaji za jimbo la Dadaab. Kwa mujibu wa UNHCR mvua hizo zilizusha mafuriko yalioeneza uharibifu mkubwa katika sehemu hiyo ya nchi.~

KM ahimiza kuwepo ushikiriano wa kimataifa kuisaidia Afrika kuepukana na umasikini

KM Kofi Annan Alkhamisi alitoa risala maalumu mjini Addis Ababa, Ethiopia mbele ya wajumbe waliohudhuria Mkutano juu ya Maendeleo ya Afrika, ambapo alionya ya kwamba pindi wahisani wa kimataifa watashindwa kushirikiana na UM pamoja na mataifa yanayoendelea kuisaidia Afrika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kuna hatari ya bara hilo kunyimwa huduma za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na, hatimaye, hata kunyimwa fursa ya kuyafikia, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Baraza Jipya la Haki za Kiutu laelekea wapi kikazi?

Hivi karibuni Baraza la Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Kiutu, lenye wajumbe wanachama kutoka Mataifa 47, lilikutana mjini Geneva, Uswiss kwenye kikao chake cha pili, ambapo kulifanyika majadiliano ya wiki tatu mfululizo kusailia mada kadha wa kadha zinazoambatana na taratibu za kuboresha utekelezaji wa haki za kiutu ulimwenguni.

Mukhtasari wa Mkutano Mkuu kusailia uharibifu wa hewa duniani

Mkutano wa 12 kwa Mataifa 189 Yalioridhia Mkataba wa Hifadhi Dhidi ya Uharibifu wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa pamoja na kuidhinisha Mkataba wa Kyoto ulianzishwa rasmi mwanzo wa juma mjini Nairobi, Kenya ambapo kulizingatiwa hatua za kudhibiti kipamoja athari za mabadiliko yaliyoletwa na uchafuzi wa hewa duniani.