Wafanyakazi wa kimataifa washindwa kuhudumia raia muhitaji katika jimbo la Sudan la Darfur
Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani katika Sudan, UNMIS, limeripoti karibuni ya kuwa wafanyakazi wa kimataifa wanaosimamia huduma za kiutu katika Darfur wanakabiliwa na vizingiti vinavyokwamisha huduma za kuwasaidia raia kupata mahitaji ya kunusuru maisha kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulio na hali ya utumiaji nguvu dhidi yao, pamoja na vitendo vya uharamia na mapigano yalioshtadi kati ya makundi ya waasi.~~