Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Risala ya nasaha ya Katibu Mkuu kwa Umoja wa Afrika(AU).

Katibu Mkuu (KM) wa Umoja wa Mataifa (UM) Kofi Annan kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU)uliofanyika majuzi katika mji mkuu wa Banjul, Gambia aliwaambia wajumbe wa Mataifa Wanachama ya kuwa anajumuika kusherehekea nao, kidhati, mafanikio ya kidemokrasia yaliyojiri miaka ya karibuni katika bara la Afrika.

Mkutano wa UM juu ya Tatizo la Silaha Ndogo Ndogo Duniani.

Mnamo mwaka 2001 wawakilishi wa Mataifa Wanachama katika UM walipitisha, kwa kauli moja, Mpango wa Utendaji uliokusudiwa kuihamasisha jamii ya kimataifa kushirikiana kuratibu kanuni mpya za kuboresha sheria za kitaifa zinazohitajika kudhibiti biashara haramu ya silaha ndogo ndogo ulimwenguni.