Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mukhtasari juu ya Mkutano Mkuu wa Pili kuhusu Maziwa Makuu

Mkutano Mkuu wa Pili juu ya Maziwa Makuu ulioandaliwa shirika na UM pamoja Umoja wa Afrika (AU), na kuhudhuriwa na Viongozi sita wa Taifa na Mkuu mmoja wa Serekali, wakiwakilisha mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda na Kenya ulifanyika wiki hii mjini Nairobi.

Baraza la Haki za Kiutu kutuma ujumbe wa uchunguzi Darfur

Baraza la UM juu ya Haki za Kiutu wiki hii mjini Geneva limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kupeleka ujumbe maalumu wa watu watano wa hadhi ya juu, katika jimbo la Darfur, Sudan ili kutathminia na kusailia hali ambayo imeripotiwa kufurutu ada katika utekelezaji wa haki za kimsingi kwa raia.

Chuo Kikuu cha Pretoria kutunukiwa zawadi ya UNESCO

Kitivo cha Haki za Kiutu cha Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini kinachosimamia mafunzo yanayohusu taratibu za kuimarisha haki za kimsingi kimetunukiwa zawadi ya dola 10,000 na Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Juhudi za Baraza Kuu kudhibiti biashara haramu ya almasi.

Mnamo mwanzo wa wiki Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio la kuunga mkono Mpango wa Kimberley na kupendekeza utaratibu huo uendelea kuimarishwa kimataifa. Kabla ya azimio kupitishwa Mataifa Wanachama 192 wa UM walisikia ripoti ya mapitio kutoka Raisi Festus Gontebanye Mogae wa Botswana, Mwenyekiti wa mwaka huu wa nchi zilizoridhia na kuidhinisha Mpango wa Kimberley.