Körösi, akunja jamvi la mjadala wa ngazi ya juu wa UNGA77
Magari yaliyotanda kuzunguka makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wakati wa wiki ya mjadala wa ngazi ya juu wa viongozi kwenye Baraza Kuu UNGA77 sasa yameondoka na barabara iliyofungwa kufunguliwa, polisi wengi na maafisa wa ujasusi ambao walizuia njia za kuelekea kwenye jengo la Umoja wa Mataifa, nao wametrejea kwenye majukumu yao ya kila siku, kilomita za vyuma vilivyokuwa vizuizi kuzunguka eneo hilo la Umoja wa Mataifa New York, vinavyojulikana kama Turtle Bay navyo vimesafirishwa kwa malori hadi kwenye maghala kusubiri hadi mwakani kwani wiki ya mjadala wa ngazi ya juu imemalizika kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa .