Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo dume katika sekta ya ardhi na kilimo bado ni kikwazo kwa lengo namba 5 la SDGs 

Mfumo dume katika sekta ya ardhi na kilimo bado ni kikwazo kwa lengo namba 5 la SDGs 

Pakua

Pamoja na uwepo wa lengo namba tano la Umoja wa Mataifa linalosisitiza kupatikana haki sawa kwa jinsia zote, hali bado ni tofauti hasa katika sekta ya ardhi na kilimo. Mfano halisi ukiwa katika maeneo mengi barani Afrika amba wanawake wanaendelea kuwa waathirika wa mfumo dume kandamizi unaowafanya kukosa haki ya kumiliki ardhi.   

Mtandao unaojulikana kama, Vuguvugu la Wakulima Wadogo Kusini na Mashariki mwa Afrika, La Via Campesina umewakutanisha wanawake wakulima wadogo kutoka mataifa 10 ya Afrika katika mjadala wa kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa wakulima wadogo walio kwenye tabaka la chini, wakijadili masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa ardhi, mjadala uliofanyika nchini Tanzania mkoa wa Morogoro katika makao makuu ya Mtandao wa Vikundi vidogo vya Wakulima Tanzania MVIWATA. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time amehudhuria mjadala huo na kuandaa makala ifuatayo. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Hamad Rashid
Audio Duration
3'58"
Photo Credit
©FAO/Luis Tato