Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaelimisha wilaya sita za Tanzania kuhusu umuhimu wa Baionuai 

FAO yaelimisha wilaya sita za Tanzania kuhusu umuhimu wa Baionuai 

Pakua

Baionuai ni muhimu sana katika sayari ya dunia ili kuhakikisha usitawi na maisha ya viumbe hai kama vile binadamu, wanyama, ndege, mimea na wadudu kwa namna nyingi. Mimea nayo husafisha hewa chafu na kuzalisha oksijeni. 

Katika kuliona hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania limewakutanisha wataalamu wa kilimo, uvuvi, mazingira, misitu na nyuki kwenye semina ya kuwajengea uwezo wananchi na wadau wa mazingira kutoka katika wilaya sita za mikoa tofautitofauti ya Tanzania ambazo ni Kigamboni, Karatu, Same, Kilolo, Mbarali na Kilosa lengo likiwa kutunza mazingira na kurejesha bioanuwai iliyopotea na kuilinda iliyopo. 

Mradi huu wa kujenga uwezo katika mikataba ya kimataifa ya mazingira, unafadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU ambapo bara la Afrika unatekelezwa katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Zimbabwe na Rwanda. Mwandshi John Kabambala wa redio washirika Tanzania Kids Time ya Mkoani Morogoro amehudhuria semina hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kabambala
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
UN Photo/ John Kabambala