Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa wa TB fuateni ushauri wa daktari kama nilivyofanya mimi na nimepona - Oduor

Wagonjwa wa TB fuateni ushauri wa daktari kama nilivyofanya mimi na nimepona - Oduor

Pakua
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO linaeleza kuwa kutokana na uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na migogoro katika mataifa mbalimbali, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kifua kikuu, TB ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo mapambano ddhidi ya ugonjwa huu yalikuwa yanaendelea vizuri. Kifua Kikuu ni ugonjwa hatari unaohitaji muda mrefu kutibu na unaweza kuwa sugu kwa dawa, lakini vile vile una kinga ambayo ni chanjo.. Thomas Oduor ni mkazi wa Nairobi ambaye aligundulika kuuugua kifua kikuu sugu mwaka 2020 na kutibiwa kwa mwaka mmoja na nusu. Na sasa miezi sita baada ya kukamilisha dozi ya dawa, afya yake inaendelea kuimarika. Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya amezungumza naye.
Audio Credit
Assumpta Massoi/Thelma Mwadzaya
Audio Duration
3'51"
Photo Credit
UNICEF/Frank Dejongh