Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mamia ya wakimbizi wa Ivory Coast na Angola warejea nyumbani:IOM

Mamia ya wakimbizi ambao walihama makwao kutokana na mzozo wa uchaguzi ulioikumba Ivory Coast wameanza kurejea nyumbani kwa usaidizi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Pia shirika hilo  linaendelea kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Angola walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia kurundi nyumbani kwa hiyari yao.

Afisa wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua kuhusu jitihada hizo alipozungumza na Monica Morara wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)

Ugonjwa wa kisukari unaweza kuzuilika:UM

Shirikisho la kimataifa la maradhi ya Kisukari IDF na shirika la afya duniani WHO wanasema maradhi ya kisukari yanaweza kuzuuilika kwa watu kuzingatia masharti ikiwemo kula vyakula vinavyofaa, kufanya mazoezi, kupungza unene na kuepuka matumizi ya tmbaku.

Leo ikiadhimishwa siku ya kisukari duniani takwimu zinaonyesha kuwa watu takribani milioni 4 wanakfa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kisukari na wengi wao wanatoka nchi za kipato cha wastani na kipato cha chini.

Burundi yasema haitavunjika moyo licha ya wanajeshi wake kuuawa Somalia

Huko Burundi, Jeshi la nchi hiyo limesema kwamba halitavunjika moyo licha ya tukio la hivi karibuni nchini Somalia ambako walinda amani wake katika kikosi cha Amisom waliuwawa wiki iliopita. Hata hivo giza linaendelea kutanda kuhusu idadi ya wanajeshi waliouwawa.

Taarifa za kutofautiana zilitolewa, Al Shabab wakidai kuwauwa wanajeshi wa Burundi zaidi ya 70 huku Jeshi la Burundi likitangaza idadi ya wanajeshi wasiozidi kumi waliouwawa.

UM wathibitisha vikosi vya Kenya kuingia Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga leo amethibitisha kwamba vikosi vya jeshi la Kenya vimeingia Somalia.

Balozi Mahiga amesema amezungumza na maafisa wa Kenya na Somalia kuhusu hatua hiyo ambayo Kenya inasema imechukua kwa ajili ya usalama na  kukabili uhalifu unaoendeshwa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-shabaab.

Tanzania yaitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada Somalia

Serikali ya Tanzania imeitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi na kunyoosha mkono zaidi kusaidia kunusuru maisha ya mamilioni ya watu nchini Somalia.

Somalia ambayo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili sasa inakabiliwa pia na tatizo kubwa la njaa, utapia mlo kwa watoto na kame.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania ameyasema hayo kwenye mdahalo uliofanyika leo nchini Tanzania na kujumuisha wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa mataifa. Mwandishi wa Idhaa hii George Njogopa alikwepo na kuandaa taarifa hii.

Nchi zinazoendelea zinahitaji msaada kukabiliana na majanga

Nchi nyingi zinazoendelea bado hazijamudu kukabiliana na athari za majanga ya asili na hata yanayosababishwa na shughuli za binadamu. Hayo yamesemwa na Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya kimataifa hii leo ya kupunguza majanga.

Mkazo umetiwa katika kpunguza athari za majanga hayo na kwenda sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Tatizo kubwa kwa mujibu mataifa yanayoendelea ni uwezo wa kukabiliana na majanga hayo yanapozuuka, utaalamu mdogo na kutojiandaa mapema.

IOM yasaidia kuwarejesha nyumbani raia wa Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasaidia maelfu ya raia wa Sudan Kusini kurejea nyumbani.

Kwa mujibu wa shirika hilo maelfu ya raia hao wengi walikuwa wamekwama katika eneo la Kosti na wengine ni wale walioishi Kaskazini kwa muda na sasa wanataka kurudi nyumbani.

Hata hivyo IOM inasema licha ya kuanza kuwasafirisha watu hao ni zoezi litakalochuka muda mrefu na linahitaji fedha, ingawa kiasi wamefanikiwa kama anavyofafanua Jumbe Omari Jumbe afisa wa shirika hilo.

Kikao kuhusu Somalia chakamilika mjini Copenhagen

Kikao cha 20 cha kimataifa cha kundi la Somalia, kimekamilisha mkutano wa siku mbili mjini Copenhagen, nchini Denmark. Mkutano huu umezungumzia mipango wa kumaliza kipindi cha mpito cha serikali ya mpito ya Somalia ifikapo Agosti 12. Mjumbe maalum wa UM nchini Somalia balozi Augustine Mahiga, alihudhuria kikao hicho wakiwemo wawakilishi kutoka Marekani na Norway. Balozi Mahiga aliongea kuhusu suala hili na redio ya UM.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)