Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Amadou Jobe, mhamiaji ambaye alirejea Gambia kutoka Ulaya, akiangalia bahari ya Pasifiki kutoka pwani ya Gambia.
UN News/ Hisae Kawamori

Sitamani tena kuzamia kwenda Ulaya: Manusura kutoka Gambia

Kila mwaka maelfu ya wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika hujaribu kufika Ulaya wakivuka bahari ya Mediterania kwa lengo la kwenda kusaka maisha bora lakini safari hiyo inaelezwa kuwa ni hatari sana kwani maelfu ya watu hufa maji au kutoweka. Evariste Mapesa anatupeleka nchini Gambia kusikia simulizi ya kijana ambaye chupuchupu apoteze maisha. 

 

Sauti
3'19"
Kina mama kutoka Kenya ambao wananyonyesha watoto wao, wakiwatumbuiza wageni kwenye uzinduzi wa wiki ya kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kunyonyesha.
UN News/Thelmaa Mwadzaya

Unyonyeshaji wa watoto maziwa ya mama huimarisha afya yao na ya mama - Wanaharakati Kenya

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, watoto wanaonyonya maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo ya uhai wanapiga hatua nzuri za kiafya kama anavyoelezea Kasha Mutenyo kwamba, "umuhimu wa kwanza wa kunyonyesha ni kwamba afya ya mtoto inaimarika na haugui kila wakati. Sio ghali, ni salama na hauhitaji vifaa vyovyote kumnyonyesha mtoto. Pia inamsaidia mama kupanga uzazi.”

Sauti
6'58"
Koketso Mukubani akisimama nje ya Kituo cha Matibabu cha Sediba Hope huko Tshwane, Afrika Kusini. Anasema wanaotumia dawa za kulevya wanapaswa kujumuishwa kwenye mipango na utekelekezaji wa kinga, tiba na huduma dhidi ya VVU na Homa ya ini C.
© UNODC

Simulizi Yangu: Kuishi na Homa ya Ini aina ya C nchini Afrika Kusini

Koketso Mokubane, mwanaume huyu raia wa Afrika Kusini alibainika kuwa na Homa ya Ini C. Amesimama nje ya kituo cha matibabu cha Sediba Hope kwenye kitongoji cha Tshwane. Koketso anafanya kazi ya kwenye ofisi ya Mtandao wa Watu wanaotumia dawa za kulevya nchini Afrika Kusini. Hili ni shirika lisilo la kiserikali linalopata msaada kupitia ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na Dawa na Uhalifu, (UNODC) kwa lengo la kutetea haki za watu wanaotumia dawa za kulevya.

Zara Bulama akiwa amebeba mmoja wa mbuzi wake aliopokea kutoka FAO katika eneo la Gongulong, Maiduguri, Nigeria, mwezi Juni 2021.
UNOCHA/Damilola Onafuwa

Katikati ya mchakato: Njia 5 zinazotumiwa na UN kuharakisha ufikiaji wa SDGs

Katika nusu ya mchakato wa hatua za kufikia ajenda kabambe ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, nchi wanachama, wavumbuzi, na washawishi wamekusanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo Jumatatu wakati Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) litakuwa linaonyesha mafanikio yaliypopatikana baada ya janga la COVID-19 katika harakati za kuelekea utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), likizindua ripoti yake ya hivi karibuni ya maendeleo.

Wadau wa lugha ya Kiswahili wakizungumza na Flora Nducha hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani.
UN News

Lengo letu ni kuhakikisha kila mtu Afrika anakijua na kukizungumza Kiswahili-Wadau

Maadhimisho ya pili ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yamewadia ni wiki ijayo tarehe 7 ya mwezi Julai ambapo wadau wote wa kiswahili duniani kuanzia kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, kwenye Mataifa wazungumzaji wa lugha hii adhimu hadi ughaibuni mambo yatakuwa bambam, lakini hapa kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa maandalizi yamefikia wapi? Na nini kitajiri? Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imewaalika wadau wa Kiswahili hapa kwenye makao makuu kufahamu maandalizi yanaendeleaje.