Tukiigeuza dunia kuwa dampo la taka basi tunajichimbia kaburi sisi wenyewe: UN
Katika kukabiliana na athari mbaya za taka kwa afya za binadamu , uchumi na mazingira leo kwa mara ya kwanza dunia inaadhimisha “siku ya kimataifa ya kutozalisha na kutotupa taka kiholela” ambayo inachagiza kila mtu kuzuia na kupunguza utupaji taka lakini pia kupigia chepuo mabadiliko ya mtazamo wa jamii kuelekea uchumi wa mzunguko.