Simulizi Yangu: Kuishi na Homa ya Ini aina ya C nchini Afrika Kusini
Koketso Mokubane, mwanaume huyu raia wa Afrika Kusini alibainika kuwa na Homa ya Ini C. Amesimama nje ya kituo cha matibabu cha Sediba Hope kwenye kitongoji cha Tshwane. Koketso anafanya kazi ya kwenye ofisi ya Mtandao wa Watu wanaotumia dawa za kulevya nchini Afrika Kusini. Hili ni shirika lisilo la kiserikali linalopata msaada kupitia ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na Dawa na Uhalifu, (UNODC) kwa lengo la kutetea haki za watu wanaotumia dawa za kulevya.