Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Wanaume na wanawake wa kiasili wa Nuñoa huko Puno, Peru, wakisuka mavazi kulingana na nyuzi za alpacas..
SGP-GEF-UNDP Peru/Enrique Castro-Mendívil

Kufadhili mustakabali bora kwa wote: Mambo 5 ya kujua kuhusu jukwaa la ufadhili wa Maendeleo

Huku uchumi wa dunia ukiendelea kuathiriwa na mfululizo wa migogoro, maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa serikali wanakutana kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa, na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 iliyokubaliwa kimataifamkwenye mstari unaostahili.

Mbu aina ya Aeded aegypti ambaye anaweza kusambaza zika, dengue au chikungunya
IAEA/Dean Calma

Je wafahamu ugonjwa wa chikungunya?

Ugonjwa wa chikungunya kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO ni ugonjwa unaonezwa na mbu jike aina ya Aedes aliyebeba virusi vya chikungunya. WHO kupitia ukurasa wake wa kuchambua magonjwa inasema kuna spishi mbili za Aedes zinasambaza ugonjwa huo ambazo ni Aedes aegypti na Aedes albopictus. Spishi hizi mbili zinaweza pia kusambaza magonjwa mengine yanayoenezwa na kama vile dengue. Mbu hawa hung’ata nyakati za mchana, ingawa wanaweza pia kung’ata asubuhi na alasiri.

Mvulana akiwa amesimama kwenye daraja juu ya mto Sanate huko Higuey, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga Fiona huko Jamhuri ya Dominika, Amerika ya Kati.
© UNICEF/Ricardo Rojas

Vimbunga: Asili ya majina hadi kuondolewa kwenye orodha

Hivi karibuni shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa duniani, WMO  kupitia kamati yake inayosimamia masuala ya vimbunga liliondoa katika orodha ya vimbunga ya kitropiki kwenye bahari ya Atlantiki majina Fiona na Ian. WMO kupitia taarifa yake hiyo iliweka bayana sababu za uamuzi huo kuwa ni madhara makubwa yaliyosababisha vimbunga hivyo huko Amerika ya Kati, Karibea, Marekani na Canada