Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

WFP Kenya

Simulizi ya Binti Armen Gakani, Mkimbizi Kalobeyei

Migogoro ya miongo na miongo nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo, DRC imefurusha watu wengi kutoka makazi yao, wengine kubaki wakimbizi wa ndani na wengnine kukimbilia nchi Jirani. Kenya ni mojawapo wa nchi ambazo zinawahifadhi wakimbizi hao na katika Kaunti ya Turkana, tunakutana na Armen Gakani, msichana mwenye umri wa miaka 23 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambaye alikimbia machafuko nchini humo na sasa yeye, akiwa na mama yake na wadogo wake wawili wenye ulemavu wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Kalibeyei. Je, ni kwa jinsi gani wameweza kujimudu kimaisha?

Sauti
5'10"
UNICEF

UNICEF na Equal Access International, wabuni mbinu za kukabiliana na changamoto katika jamii

Janga la tabianchi limesababisha kupotea kwa upatikanaji wa elimu, huduma muhimu, na ajira kwa vijana nchini Kenya. Hata hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Equal Access International wamewawezesha vijana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa ufahamu kuhusu suluhisho la kukabiliana na tatizo hilo. Evarist Mapesa wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anatufafanulia zaidi katika Makala hii.

Sauti
3'37"
Frida Jausiku

Mshtakiwa ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia – Ibara 11

“Kila mtu aliyehukumiwa kwa kosa la adhabu ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa ana hatia kwa mujibu wa sheria katika kesi ya hadhara ambapo amekuwa na dhamana zote zinazohitajika kwa ajili ya utetezi wake, na Hakuna mtu atakayepatikana na hatia ya kosa lolote la adhabu kwa sababu ya kitendo au kutotenda jambo ambalo halikuwa ni kosa la adhabu, chini ya sheria ya kitaifa au kimataifa, wakati lilipotendwa, wala haitatolewa adhabu kubwa kuliko ile ambayo ilitumika wakati kosa la adhabu lilipotendwa.” Linasema tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo m

Sauti
3'48"
UN News/Thelma Mwadzaya

Makala: Je akili mnemba AI ni faida au athari katika sekta ya filamu?

Hii leo makala inamulika Akili Mnemba au AI ambayo imebadili fani mbali mbali ikiwemo ya sanaa. Ni kwa kutambua umuhimu wa suala hili shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mjadala maalum kuhusu akili mnemba kwenye sekta ya filamu unaoendelea huko Paris Ufaransa. Ajenda inajikita ni manufaa na changamoto kwa sekta ya sanaa ukizingatia maadili  na ubunifu. Yvonne Muinde mchanganya picha za filamu ni msanii aliyebobea kwenye sekta ya ubunifu na dijitali na mshiriki wa mjadala huo wa UNESCO ulioanza jana.

Sauti
5'51"
UN News

Asante FAO kwani sasa nimeweza kujipatia zaidi ya dola Elfu 3 kupitia kilimo cha kisasa

Wanawake wa vijijini wanatambuliwa kimataifa kupitia siku yao ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 mwezi Oktoba. Mwaka huu maadhimisho yamefanyika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania, huko Afrika Mashariki. Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula, FAO liliandaa tukio maalum la kutambua mchango wa wanawake hao hasa kwa kuzingatia mchango wao katika uzalishaji chakula, kwani shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO linasema wanawake ni zaidi  ya asilimia 40 ya nguvukazi kwenye sekta ya kilimo.

Sauti
4'45"
UN News

Tanzania tumepiga hatua kubwa kupambana na kifua kikuu: Waziri Ummy Mwalimu

Kifua kikuu au TB ni moja ya changamoto kubwa za kiafya duniani na janga ni kubwa zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO duniani kote, TB ni sababu ya 13 inayoongoza kwa vifo na ya pili muuaji wa magonjwa ya kuambukiza baada ya COVID-19 ikiwa juu ya VVU na Ukimwi. Shirika hilo linakadiria kwamba mwaka 2021, takriban watu milioni 10.6 waliugua kifua kikuu kote duniani wakiwemo wanaume milioni sita, wanawake milioni 3.4 na watoto milioni 1.2.

Sauti
3'39"
UPU

UPU na harakati za kusaidia nchini kusongesha posta za kidijitali

Leo ni siku  ya posta duniani ambapo maudhui ni Pamoja kwa kuaminiana:Ushirikiano kwa mustakabali salama na uliounganika. Lengo la maudhui hay ani kuchagiza serikali na huduma zao za posta kusaidia maendeleo ya posta ya kidijitali ambayo itaboresha mtandao wa kale wa posta ulioendelezwa karne na karne, ukihitaji kwa kiasi kikubwa mtoa huduma na mhudumiwa kuonana uso kwa uso, jambo ambalo sasa kwa kiasi kikubwa limebadilika, huduma za posta mtandao zikichukua fursa.

Sauti
5'37"
© UNICEF/UNI404964/Zuniga

Madarasa yajengwa Sofala, Msumbiji kuhimili majanga ya asili ikiwemo vimbunga

Hii leo Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ya kwanza ya uchambuzi wa aina yake kuhusu matukio ya watoto kulazimika kukimbia makwao kutokana na majanga yasababishwayo na hali ya hewa ikisema zaidi ya watoto milioni 43 walijikuta wakimbizi wa ndani kwenye nchi 44 katika kipindi cha miaka sita iliyopita, ikitafsiri kuwa ni watoto 20,000 kila siku.

Makadirio ya ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, yanaonesha kuwa kufurika kwa mito pekee kutafurusha watoto milioni 96 katika miaka 30 ijayo.

Audio Duration
4'41"
ILO

Simulizi ya kijana mkimbizi Gad Harindimana Mnyarwanda nchini Uganda - FAO inavyofungua uwezo

Makala inatupeleka nchini Uganda kumsikiliza Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi Nakivale mnufaika wa programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO kupitia shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation. Gad Harindimana amepata kazi ya ufundi pikipiki baada ya kukamilisha programu ya Huduma hizo. Anasimulia kwa lugha ya Kinyakole inayotafsiriwa na Anold Kayanda. 

Sauti
3'51"