Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante FAO kwani sasa nimeweza kujipatia zaidi ya dola Elfu 3 kupitia kilimo cha kisasa

Asante FAO kwani sasa nimeweza kujipatia zaidi ya dola Elfu 3 kupitia kilimo cha kisasa

Pakua

Wanawake wa vijijini wanatambuliwa kimataifa kupitia siku yao ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 mwezi Oktoba. Mwaka huu maadhimisho yamefanyika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania, huko Afrika Mashariki. Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula, FAO liliandaa tukio maalum la kutambua mchango wa wanawake hao hasa kwa kuzingatia mchango wao katika uzalishaji chakula, kwani shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO linasema wanawake ni zaidi  ya asilimia 40 ya nguvukazi kwenye sekta ya kilimo. Ingawa hivyo tija itokanayo na kilimo hicho mara nyingi huwa ni ya chini sana na ndio maana FAO nchini Tanzania kupitia Mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP, wameendesha miradi kama vile kilimo cha kisasa kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, halikadhalika  ufugaji wa kisasa. Baadhi ya wanawake wanufaika wa miradi hiyo wamekuwa mashujaa wa chakula, maudhui ya siku hiyo ya mwanamke wa Kijijini. Sasa wamefanya nini? John Kabambala wa Radio Washirika Kids Time FM ya mkoani Morogoro nchini Tanzania alikuwa shuhuda wetu wa tukio hilo mkoani Kigoma. 

Audio Duration
4'45"
Photo Credit
UN News