Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/Anold Kayanda

MuDa Africa washindi wa ufadhili wa UNESCO wahamasisha wasichana kutoficha vipaji vyao

Wasanii kutoka Taasisi ya Muda Africa ya nchini Tanzania, kundi ambalo ni washindi wa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wanatoa wito kwa wasichana na wanawake kutoficha vipaji vyao ili waweze kutimiza ndoto zao na jamii iwasaidie kuyatimiza malengo hayo kwani hiyo itasaidia kuondoa pengo la usawa wa kijinsia katika tasnia mbalimbali ambazo kwa muda mrefu zinahodhiwa na wanaume.

Sauti
4'4"
UNICEF

Hakikisho la maji safi na salama lachochea jamii kuishi na utangamano Mkoani Kigoma nchini Tanzania

Ufumbuzi wa ubunifu wa maji unaotumia teknolojia ya nishati ya jua ambao unafanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wake ukiwemo ule wa utekelezaji, Water Mission, na ule wa kutoa msaada wa fedha Grundfos Foundation kutoka nchini Denmark umesaidia serikali ya Tanzania kubuni suluhisho la msingi na la kudumu la maji katika jamii 15 za mkoa wa Kigoma ulioko magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Lengo lao kubwa ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa watu 99,107 mkoani humo ifikapo Machi 2024. 

Sauti
5'48"
UN News/Assumpta Massoi

Vijana ni wakati wetu sasa kufanikisha upatikanaji wa maji- Laurel

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ulifanyika kwa siku tatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuanzia tarehe 22 mwezi huu wa Machi. Mkutano huu ulichukuliwa kama fursa ya kipekee ya kizazi hiki ya kuharakisha maendeleo kuelekea upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira ifikapo mwaka 2030 kwa kuzingatia kuwa mara ya mwisho ya mkutano kama huu kufanyika ilikuwa mwaka 1977.

Sauti
4'48"
UN News/ George Musubao

Vikosi vya usaidizi wa haraka nchini DRC kutoka Tanzania vyakabidhiana majukumu

Mashambulizi dhidi ya raia huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yanaripotiwa kila uchao ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini  humo, MONUSCO unaendelea kujiimarisha ili kuimarisha pia usalama wa raia ambalo ndilo jukumu lake. 

Harakati za kulinda raia na kukabiliana na waasi zinaendeshwa na walinda amani kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo Tanzania ambapo hivi karibuni kikundi kipya cha kutoa usaidizi wa haraka kimewasili kuendeleza jukumu la kikundi cha awali. 

Sauti
3'42"
UN News

Wasichana wapatiwe haki zao za elimu bora na wajengewe uwezo wa teknoljia - Elionaora

Kikao cha 67 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW67 kielekea tamati, mwaka huu 2023 kikiwa kimebeba mada uvumbuzi, mabadiliko ya kiteknolojia, na elimu katika zama hizi za kidigitali kwa ajili ya kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote. Mijadala mingi katika mkutano huu imelenga kuwawezesha na kuhakikisha watoto wa kike wanaingia kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati au STEM ili hapo baadaye waweze kuchangia katika ubunifu wa teknolojia katika enzi hizi za dunia ya kidijitali. 

Sauti
5'25"
UN NEWS/ Anold Kayanda

Tumejadili mambo mengi katika Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani - Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson.

Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani ulioanza tarehe 11 mwezi huu wa Machi na kujumuisha Mabunge ya Nchi Wanachama, Waangalizi wa Kimataifa na Majukwaa mbalimbali ya Kibunge ili kuchagiza Amani na kujenga Jamii Jumuishi na Kuvumiliana umehitimishwa leo tarehe 15 Machi 2023. Katika Mkutano huu Mabunge yameeleza namna ambavyo yameweza kufikia ushirikishwaji wa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla katika kulinda amani sambamba na kusisitiza kuheshimu mipaka ya kila mmoja wao. Dhima hii ni msisitizo wa malengo ya Maendeleo Endelevu hususani lengo namba 16 la Umoja wa Mataifa.

Sauti
4'20"
UN News

Mitandao ya intaneti kwenye ngazi ya jamii ndio jawabu la kufikisha teknolojia kwa walio pembezoni- Bi. Lugangira

Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 ukiendelea na maudhui makuu yakiwa ni namna ugunduzi na teknolojia ya dijitali inaweza kuchangia kumkwamua mwanamke, Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa nayo inaendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu kule watokako hali iko namna gani na nini kinafanyika ili kuhakikisha teknolojia ya kidijitali inatumika kivitendo badala ya kusalia kwenye makabrasha au kumilikiwa na wachache na hivyo kuzidi kuongeza pengo la kidijitali. 

Sauti
4'40"
Credit: TANZBATT9/ Denisia Lihaya

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania huko DRC wakabidhiana lindo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walinda amani kutoka Tanzania kikosi cha 9 wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wanaendelea kushika doria na kulinda raia katika jimbo la Kivu Kaskazini ambapo wiki hii kikosi cha 9, TANZBATT 9 kimemaliza muda wake na kukabidhi majukumu kwa kikosi cha 10, TANZBATT 10. Je nini kimejiri katika makabidhiano hayo ? Kapteni Denisia Lihaya, Afisa habari wa TANZBATT 9 kabla ya kurejea nyumbani ametuandalia ripoti  hii ya makabidhiano. 

Sauti
4'9"