Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Photo/Violaine Martin

Fulgence Kayishema, Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari huenda atahukumiwa nchini Rwanda - Serge Brammertz

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania, Serge Brammertz ameeleza kuwa Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei 24 huko Paarl nchini Afrika Kusini huenda akapelekwa nchini Rwanda kukabiliana na mkono wa sheria kutokana na tuhuma za kushiriki kuwaua watu zaidi ya 2000 wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Sauti
4'47"
ITU

Huduma za fedha mtandao zamwondolea mwanafunzi adha ya kufuata fedha benki

Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo. Ukosefu wa huduma za fedha kimtandao zinakuwa kikwazo kwani wananchi hupoteza muda mwingi benki kusubiria malipo ambayo wangaliweza kuyapokea kupitia simu za kiganjani au rununu.

Audio Duration
3'41"
GLAMI Tanzania

Mradi wa Binti Shupavu wasongesha SDG4 nchini Tanzania

Nchini Tanzania Shirika la lisilo la kiserikali la Girls Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI) kupitia Mradi wake wa Binti Shupavu, unaowajengea Stadi za Maisha ikiwemo uwezo wa kujitambua, mabinti walioko Shule, unaendelea na juhudi za kufanikisha Lengo la Nne la maendeleo endelevu SDG’s linalohusu Elimu, ambapo Jumla ya wasichana 824 wananufaika kutoka katika Shule Tisa zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo Mwezi huu wa Tano limekamilisha Programu ya kufanya vikao na wazazi katika Shule hizo ili kuwajengea uwezo wa malezi ya watoto wao.

UNICEF Kenya

Makala: Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya

Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ukifanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine,lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya  ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.

Sauti
4'13"
UN News/George Musubao

Ingawa kuna changamoto najitahidi kutunza familia yangu- Tsinduka

Hii leo ni siku ya kimataifa ya familia duniani ambapo maudhui ya mwaka huu ni mienendo ya makundi ya watu na familia wakati huu ambapo idadi ya watu inaongezeka ingawa kwa kiwango cha chini. Umoja wa  Mataifa unasema kupungua kwa idadi ya wanafamilia hutoa fursa ya familia kupatia huduma bora zaidi watoto, mathalani elimu na afya.

Sauti
4'26"
Stella Vuzo/UNIC Dar es Salaam

Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew kuwawakilisha vijana wa Tanzania katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu.  

Wakati wa mkutano huu wa juu kabisa katika Diplomasia ya Umoja wa Mataifa, vijana pia hushiriki katika mikutano ya kando ili kuchangia mawazo yao katika mstakabali wa ulimwengu.  

Vijana wawili kutoka Tanzania Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew watawakilisha vijana wenzao wakati wa Baraza hili.  

Sauti
2'37"
© UNICEF/Veronica Houser

Jamii msimkatae msichana akipata ujauzito bila kutarajia. Si mwisho wa maisha - Ashley Toto

Ripoti iliyopewa jina Kuzaliwa kabla ya wakati: muongo wa hatua dhidi ya kuzaliwa kabla ya wakati, iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia Afya ya Mama, watoto na vijana inaeleza kwamba mwaka 2020 takriban watoto milioni 13.4 duniani walizaliwa kabla ya wakati yaani njiti, huku karibu milioni 1 kati yao wakifariki kutokana na matatizo yanayotokana na hali hiyo ya kuzaliwa kabla ya wakati. 

Sauti
4'44"