Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wanajeshi walinzi wa UM waachiwa huru nchini Congo-DRC.

Wanajeshi watano walinzi wa amani wa UM kutoka Nepal waliotekwa nyara na kundi la waasi la FNI katika JKK kuanzia tarehe 28 Mei (2006) waliachiwa huru majuzi wakiwa na afya zao imara. Wanajeshi hawa hivi sasa wameshajiunga na vikosi vya kuimarisha amani vya UM ili kujiandaa na kusimamia hali ya utulivu ndani ya nchi kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa mwisho wa mwezi.~~

Ripoti ya KM kuhusu mzozo nchini Uganda Kaskazini.

Ripoti ya KM iliyowasilishwa karibuni kuhusu mzozo wa Uganda ya Kaskazini imesisitiza ya kuwa licha ya Serekali za mataifa jirani kujaaliwa uwezo na dhamana ya kukabiliana na utenguzi wa haki za kiutu unaoendelezwa na kundi la waasi la LRA dhidi ya raia, kwa wao kuweza kulidhibiti tatizo hilo kithabiti na kusawazisha usalama wa eneo, watahitajia vile vile msaada na ujuzi wa UM.~~

Jean-Marie Guehenno awaarifu waandishi habari juu ya vikosi vya UM kwa Darfur.

Makamu KM juu ya Operesheni za Amani za UM, Jean-Marie Guehenno aliwaarifu waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu kwamba ni muhimu kwa jamii ya kimataifa kufanyisha mazungumzo ya hali ya juu na Serekali ya Sudan ili kuondosha hali ya kutofahamiana na kutoaminiana, pindi tumenuia kuwasilisha mafanikio ya kudumu kuhusu pendekezo la kutuma majeshi ya amani ya UM katika Darfur, Sudan.

Mwakilishi wa KM juu ya Usomali ajadilia mchango wa UM nchini.

Mwakilishi wa KM juu ya Usomali, Francois Lonseny Fall wiki hii aliwaarifu waandishi habari wa kimataifa ya kuwa lengo kuu la UM katika Usomali ni kuwahimiza wafuasi wa makundi ya Kiislamu na wawakilishi wa Serekali ya Mpito (TFI) kuendelea kujadiliana na kushauriana juu ya uwezekano wa kurudisha, kipamoja, salama na amani katika taifa lao.~~

Mpango wa Utendaji wa UM Kudhibiti Silaha Ndogo Ndogo Wafanyiwa Mapitio

Miaka mitano baada ya Umoja wa Mataifa (UM) kupitisha Mpango wa Utendaji wa kukabiliana na biashara haramu ya silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi katika dunia, Makao Makuu ya UM yalishuhudia mkusanyiko wa hali ya juu wa wawakilishi karibu 2,000 wa kimataifa kutoka serikali wanachama mbalimbali, pamoja na mashirika ya kikanda na kimataifa kwa makusudio ya kuzingatia uwezekano wa kulikomesha tatizo la kuenea kwa silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi katika ulimwengu.