Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Somalia

Mwanamke akipita kwenye maji ya mafuriko katika Jimbo la Hirshabelle, Somalia.
© WFP/Arete/Abdirahman Yussuf Mohamud

OCHA na wadau waanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi. 

Sauti
2'17"
Pwani ya Mogadishu, nchini Somalia
UNODC/Jeremy Douglas

Viongozi wa OCHA na FAO kuadhimisha siku ya wanawake duniani nchini Somalia

Ziara ya Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA Bi. Joyce Msuya na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO Beth Bechdol nchini Somalia imewaonesha namna takriban watu milioni 7 walivyo na uhitaji wa msaada wa haraka wa kuokoa maisha kutokana na kuathirika na njaa, vita na mabadiliko ya tabianchi.