Wadau wa kimataifa watoa wito wa utulivu Garowe Somalia baada ya majeshi kuanza kukusanyika: UNSOM
Wadau wa kimataifa watoa wito wa utulivu Garowe Somalia baada ya majeshi kuanza kukusanyika: UNSOM
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM kwa ushirilkiano na wadau wengine wa kimataifa wamesema wana wasiwasi mkubwa kuhusu hatari ya mivutano zaidi ikiwemi hali ya sasa ya kukusanya majeji huko Garowe.
UNSOM imesema kukusanyika huko kwa majeshi Garowe kunatisha raia na kumesababisha kufungwa kwa shule.
UNSOM imesisitiza kwamba “Hakuna kinachohalalisha machafuko au tishio la kutumia nguvu. Madai yote yanapaswa kushughulikiwakwa njia ya amani na kupitia majadiliano. Tunatoa wito kwa pande zote kushughilkia tofauti zao kupitia njia za amani”
Taarifa hiyo ya Pamoja imesema wadau wa kimataifa wanaenendelea kuiungamkono na kuisaidia Somalia na watu wake katika kujenga msingi kwa ajili ya amani ya kudumu na mustakbali bora kwa jamii nzima.
UNSOM imesema “Tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali na tunatoa wito wa kuacha mivutano mara moja na kuanzisha haraka mazungumzo ya kisiasa na viongozi wengine wa kijamii.”