Mapigano yameanza tena katika maeneo kadhaa ya miji ya Masisi, Rutshuru na Sake DRC
Wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanasema wana wasiwasi mkubwa kutokana na kuzorota kwa kutisha kwa hali ya kibinadamu huko Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaeleza wanahabari leo Mei 31 jijini New York, Marekani.