Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MUHTASARI WA HABARI: GAZA, DR CONGO, MAANDAMANO MAREKANI

Waandamanaji waandamana nje ya chuo kikuu cha Columbia mjini New York.
UN Photo/Evan Schneider
Waandamanaji waandamana nje ya chuo kikuu cha Columbia mjini New York.

MUHTASARI WA HABARI: GAZA, DR CONGO, MAANDAMANO MAREKANI

Amani na Usalama

Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”

DR Congo

Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Katika ukurasa wake wa X hii leo shirika hilo limesema jimboni Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini pekee watu milioni 5.4 hawana uhakika wa chakula, milioni n6.4 ni wakim bizi wa ndani na wagonjwa wa kipindupindu kwa mwaka huu pekee wamefikia 8,200. OCHA imeongeza kuwa sasa dola bilioni 1.48 zinahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa watu zaidi ya milioni 4.

Maandamano Marekani

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema anatatizwa na mlolongo wa hatua nzito zinazochukuliwa kutawanya na kusambaratisha maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani.

Kupitia tarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Bwana Türk amesisitiza kuwa "Uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani ni jambo la msingi kwa jamii  hasa wakati kuna kutokubaliana vikali juu ya masuala makubwa, kama vile ilivyo sasa ikihusiana na mzozo unaoendelea katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel,".