Neno la Wiki- Paraganyika
Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na anafafanua neno 'Paraganyika'.
Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na anafafanua neno 'Paraganyika'.
Leo mchambuzi wetu ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anafafanua neno ambalo hutumika ndivyo sivyo“ Mgeni wa heshima."
Katika kujifunza Kiswahili, Mchambuzi Onni Sigalla wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania “BAKITA” anachambua maana na matumizi ya neno “AGHALABU” ambapo anaeleza maana mbili za neno hilo. Tofauti na ile iliyozoeleka kwa matumizi ambapo neno aghalabu hutumiwa kueleza utokeaji wa mara kwa mara wa jambo, mtaalam huyo ameongeza maana nyingine isiyofahamika sana inayohusishwa na kundi la watu katika jamii au jumuiya.
Neno la wiki limejikita katika kuichambua methali isema, 'Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto'. Mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora anasema methali hii kimsingi inaeleza dhana ya kuwa ikiwa mtu ana mazoea fulani au kazoea mazingira fulani, hayamtishi, atatekeleza analolitekeleza bila kuogopa.
Aida Mutenyo, mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anachambua matumizi ya neno TAFADHALI. Anasema kuwa nchini Uganda neno hili ni moja ya maneno yanayowasumbua wazungumzaji wa kiswahili kwani wanalichanganya na neno AFADHALI.
Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na anafafanua matumizi ya neno Asilani.
katika Neno letu wiki hii mchambuzi wetu ni Mwahija Ali Juma ambaye ni katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar , BAKIZA anafafanua maana ya maneno “SAINI” na “SAHIHI.”
Katika NENO LA WIKI hii leo mchambuzi wetu Ken Walibora, mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA anachambua methali Kizuri hakikosi ila. Walibora anasema katika jamii yoyote ile hata kama mtu awe mzuri namna gani lazima ana kasoro na ndipo matumizi ya neno ila.
Na sasa ni neno la wiki ambapo Bi. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anachambua maneno KUFA na KUFARIKI. Bi. Mwanahija anasema kwa kawaida kufa linaweza kutumika kwa mnyama au binadamu. Hata hivyo kufariki ni kwa binadamu peke yake na inapendeza zaidi tukisema kufariki dunia.
Katika Neno la Wiki linachambuliwa neno MEZA.
Na mchambuzi wetu kwa leo ni Aidah Mutenyo Mwenyekiti wa idara za kiswahili katika vyuovikuu Afrika Mashariki