Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha ya UNAMA/Fardin Waezi

Wananchi wana wajibu mkubwa wa kuepusha majanga: UN

Ajenda ya malengo ya maendeleo enedelevu SDGs ya mwaka 2030 inahimiza serikali, asasi zakiraia na mashirika ya kibinadamu kuweza kupigia chepuo  suala la ulinzi wa mazingira ili kuepuka majanga kama nvua za kupindukia, vimbunga, mafuriko na kadhalika. Mwandishi wetu kutoka maziwa makuu Ramadhan Kibuga leo ametembelea eneo la Gatunguru nje kidogo ya jiji la Bujumbura Burundi, na kushuhudia athari za tatizo la mvua kubwa za kila wakati na kusababisha maporomoko ya ardhi.

Sauti
4'1"

Vijana nchini Zambia ni mfano wa kuigwa katika kilimo

Ufugaji samaki ni biashara inayo wakwamua vijana wengi nchini Zambia na tatizo la ajira. Shirika la kazi duniani ILO na lile chakula na kilimo FAO kwa pamoja na serikali ya Zambia wameanzisha mradi wa kuwawezesha vijana vijijini kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali katika kilimo na ufungaji, ikiwa ni mpango wa malengo ya maendeleo endelvu ya mwaka 2030 katika kutokomeza umasikini.

Sauti
44"
UN News/Assumpta Massoi

Sisi ni warendile tutambulike tulivyo: Alice

Yaelezwa kuwa utamaduni ni kielelezo cha ustawi wa kila jamii. Utamaduni hudhihirishwa kwa njia mbalimbali iwe lugha, mila, mavazi, chakula na kadha wa kadha. Kutotambulika kwa utamaduni wa mtu au jamii ina maana ni kutokomea kwa jamii hiyo na ndio maana jamii ya warendile walioko kaunti ya Marsbit nchini Kenya wanapaza sauti ili kabili hilo litambuliwe kwa kina ili hata mila zao basi ambazo si potofu ziweze kutumiwa katika kusongesha maisha si tu kwenye jamii zao bali pia kwingineko ambako zinafaa.

Sauti
3'48"

Samaki wametoweka kwasababu ya uvuvi haramu

Serikali nyingi duniani zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za uvuvi haramu ambao mara nyingi huathiri mali asili ya baharini na kusababisha hasara kubwa kwa serikali, na pia  kuathiri mapato ya  wavuvi ambao hufuata sheria ya uvuvi.

Mwandishi wetu John kibego amefuatilia kwa ukaribu changamoto za uvuvi haramu katika ziwa Albert, katika wilaya ya Bulisa nchini Uganda ambapo wavuvi haramu wamekuwa wakivua kinyume cha sheria na kusababisha hasara kubwa katika mapato ya serikali ya kijiji.

Je nini kilichojiri ?ungana naye katika makala hii.

Sauti
3'35"

Pale Mmaasai mwanaume anapopigia chepuo haki za wamasai wanawake

Ni kawaida kwa mtu anayeamua kusimama kidete dhidi ya mila zinazopigiwa chepuo na wenzake kukumbwa na misukosuko! Na ni misukosuko zaidi pindi mtu huyo ni wa kabila la kimasai na ni mwanaume anayetetea haki za wamasai wanawake na wasichana wanaokumbana na mila potofu kama vile ukeketeji na kupokwa ardhi zao pindi mume anapofariki dunia. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Alais Esoto, mratibu wa shirika la kiraia la Naserian huko Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania. Alikumbana na mengi lakini hakukata tamaa na sasa ameona matunda.

Sauti
4'22"
Picha na FAO

Watoto Kenya nao wahifadhi mazingira

Serikali ya Kenya inaendesha  kampeni ya uhifadhi wa mazingira, ambapo elimu ya upandaji miti inatolewa katika shule za msingi ili kuelimisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa  manzingira.

Katika makala hii, mwandishi wetu Patrick Newman anatukuletea harakati za vijana wa shule za msingi mashariki mwa Kenya waliopanda miti wakati walipohitimu shule ya msingi mwaka 2012.

Sauti
3'8"
Picha: UM/Video capture

Muziki wabadili mtazamo wa wakimbizi wa CAR

Tangu mwaka 2013, mamia ya maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamelazimika kukimbia makazi yao kufuatia vurugu na mauaji ya kikatili yanayotekelezwa na wapiganaji nchini humo.  Watu zaidi ya 180,000 wamekimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, moja ya nchi zilizo masikini zaidi duniani.

Sauti
3'56"